| 
||
| Mwanahabari wa Habari leo Iringa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard akitoka kutazama Kimondo | 
| Mgeni akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya | 
| Wanahabari wakitoka katika Kimondo kulia na Slvanus Kigomba (ITV) na kulia ni Iren Mwakalinga (TBC),nyuma yao ni ofisi ya makumbusho hayo | 
| Mhifadhi akionyesha jiko ambalo linatumika eneo hilo | 
| Nyumba ya wahifadhi wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya | 
| Mhifadhi msaidizi wa makumbusho ya Kimondo akiingia katika nyumba yake | 
| Hii ndio nyumba ya mhifadhi mkuu na mhifadhi msaidizi wa Kimondo Mbeya | 
| Mwanahabari wa ITV Iringa Slvanus Kigomba akijipumzisha kando ya Kimondo | 
Mwanahabari  wa Star Tv Iringa  Mawazo Marembeka  kushoto akiwa na mzee  wa matukiodaima katika Kimondo
| Wanahabari wakimhoji mhifadhi msaidizi wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya Bw Mussa Nsojo | 
| Hiki ndicho kimondo kina tani 12 | 
| Afisa utalii kanda ya kusini Tanapa Bi Risala Kabongo akiwa katika kibao cha Kimondo | 
MKOA  wa  mbeya   umepania  kuboresha miundo  ya  kituo cha mambo ya  kale  cha  Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa  iwapo Idara ya Mambo ya kale iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali  ombi la mkoa   huo  kukabidhi  kivutio  Halmashauri  ya  Mbozi.
Hatua hiyo   imekuja  kufuatilia ziara ya  wanahabari  mkoani Iringa
wanaotembelea vivutio vya utalii mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa kama njia ya kuhamasisha utalii mkoa ya nyanda za juu kusini na pia kubaini sababu za utalii kutokua kwa kasi katika mikoa hiyo .
wanaotembelea vivutio vya utalii mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa kama njia ya kuhamasisha utalii mkoa ya nyanda za juu kusini na pia kubaini sababu za utalii kutokua kwa kasi katika mikoa hiyo .
Mhifadhi msaidizi  wa  kituo  cha makumbusho ya  mambo ya kale ya  Kimondo wilayani  Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema  kuwa  mbali  ya  watalii wengi kupenda  kutembelea  eneo  hilo la Kimondo ila miundo  mbinu ya  eneo hilo si rafiki kwa  watalii kuendelea  kutembelea  kutokana na serikali  kushindwa  kuboresha  majengo na  eneo  hilo kwa  ujumla.
Alisema kuwa  kimondo  hicho  ambacho mwaka kilipoanguka  eneo  hilo
haufahamiki ila utafiti wake ulianza kati ya mwaka 1930 -1931 na
kubainika kuwa si jiwe la kawaida bali ni sayari iliyoanguka kutoka angani toka wakati huo kimendelea kupata umaarufu wa watalii kufika kutembelea eneo hilo japo katika eneo hilo mazingira yake ni mabovu zaidi.

Mhifadhi huyo  akielezea  historia  ya  kimondo  hicho  alisema  kabla  ya watafiti  kubaini  kuwa ni  kimondo miaka  ya  nyuma kulikuwa na wenyeji  ambao walikuwa  wakiishi  eneo  hilo na  mkazi  mmoja aliyefahamika  kwa jina la Harele  ambae  alikuwa akifanya kazi  ya uhunzi kuweza kubaini jiwe  hilo la ajabu wakati akitafuta  udongo chuma kabla  ya  kumega kipande  kidogo na kutengenezea shoka .
Alisema kutokana na wakati   huo chuma kuwa na dhamani  kubwa alipeleka taarifa  kwa chifu  wa  eneo  hilo na  kulifanya  eneo hilo  kuwa  la tambiko kabla utawala  wa Waingereza  kuchukua eneo  hilo na kulihifadhi kabla  ya  serikali ya  Tanzania  kupitia idara ya mambo ya kale  kuhifadhi  eneo  hilo.
Kuhusu changamoto  kubwa  zilizopo eneo  hilo alisema ni pamoja na kukosekana kwa  nyumba  bora  za watumishi ,jengo la ofisi  ya makumbusho  kutokana na kibanda  kilichopo  kutokuwa na sifa ya utalii ,pia miundo mbinu  ya barabara  kufika  kituoni hapo.
Afisa utalii ofisi ya utalii kanda  ya kusini Bi Risala Kabongo akielezea kivutio   hicho  alisema  kuwa  ni  moja kati ya  vivutio  visivyo  vya kawaida  hapa  nchini na kuwa  iwapo  serikali itaboresha  zaidi  eneo hilo upo uwezekano  wa uchumi  wa  mkoa  wa Mbeya kukua  zaidi  kupitia kivutio  hicho .
”
Kivutio hiki kinavutia zaidi ila ushauri wangu kwa serikali ni
kuboresha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na kutenga eneo la banda la
wageni na eneo la kujenga mahema kwa wageni…..Kimondo hiki kimetoka katika sayari ya Mars na hivyo ni kivutio cha ajabu zaidi”

Katibu tawala msaidizi (miundombinu)  mkoa  wa  Mbeya  Kastory Msigala alisema  kuwa mkoa  huo  kupitia  kikao  chake  cha kamati ya ushauri ya  mkoa  kimeiandikia  barua  idara ya mambo ya kale  ili kuipa eneo hilo  la Kimondo Halmashauri ya  Mbozi  ili  kusimamia kwa lengo la kuiboresha  zaidi.
Kwani alisema  shida  kubwa ya  Halmashauri  hiyo na mkoa  kushindwa
kuboresha majengo na miundo mbinu inayozunguka makumbusho hayo ni kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kutokana na usimamizi wa eneo hilo kuwa chini ya idara ya mambo ya kale ila pale idara hiyo itakapokabidhi katika serikali ya wilaya upo uwezekano wa wilaya kusimamia vizuri zaidi.

Alisema katika mkoa   huo kuna  jumla  ya  vivutio 13  vilivyotambuliwa kikiwemo  kivutio   hicho  cha Kimondo  na  kuwa mbali ya  vivutio hivyo  bado  mkoa  umejipanga zaidi  kutangaza  utalii  kufuatia ushirikiano mkubwa  uliopo kati ya  mkoa huo na ofisi ya SPANEST  , bodi ya utlii ,wizara  ya utalii na wadau mbali mbali  kukuza  utalii mkoani  humo .
No comments:
Post a Comment