Meneja
 wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu 
masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa 
Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika 
katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya 
kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na 
Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous jana
Maelezo kuhusu masalia ya  injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge
Waziri
 Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya 
kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya 
wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo 
Waziri
 Nyalandu akisalimiana na Ofisa Mawasiliano na Umma wa Ubalozi wa 
Marekani nchini Tanzania,  David Feloemann, alipowasili kwenye mbuga ya 
Selous jana
![]()  | 
| Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous | 
Balozi
 wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini
 na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa 
Ujerumani  Egon Kochanke
Balozi
 wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa 
Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa 
Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa 
wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga
 ya wanyamapori ya Selous jana. 
 Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark 
Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani 
Egon Kochanke
 Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania  
Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa 
Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika 
mbuga ya wanyama ya Selous jana
Waziri
 Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya kubadilishana 
hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress
Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani 
 Vifaa
 mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na 
Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya 
wanyamapori ya Selous
 Askari
 wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni 
vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Seriali za Marekani na Ujerumani
 kwa ajili ya kukabiliana na ujangili
Askari
 wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa
 vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya 
kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha 
zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

 
 






No comments:
Post a Comment