TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 23, 2015

YAH: KUVUNJIWA NYUMBA KWA GHAFLA NA MH. DIWANI WA KATA YA MIANZINI MBAGALA

unnamed (10) unnamed (11) unnamed (13)
Mimi mtajwa hapo juu ni mwandishi wa habari ninayefanya kazi katika gazeti la Sani kwa miaka minne sasa nikiwa kama Mwandishi wa habari Mwandamizi na mpiga picha.
Ninayo masikitiko makubwa kufuatia kitendo cha Mkurugenzi na mmiliki wa Gazeti la Sani ambaye pia ni Mh. Diwani Athuman Bawj Mbwana wa kata ya Mianzini, Mbagala Temeke kuchukua hatua za kuivunja nyumba niliyokuwa naishi kwa ghafla huku familia yangu ikiwa ndani hivyo kuniacha bila mahali pa kuishi na kuruhusu mali zangu kuibiwa vikiwemo vitendea kazi.
Tukio hili alifanya Januari 19 majira ya saa 9 alasili ambapo bila kuwa na kibali chochote, wala idhini ya Serikali ya Mtaa, mjumbe au usimamizi wa Polisi na pasipo kunipa Notice Mheshimiwa huyo alivamia nyumba hiyo na kuivunja huku familia yangu ikiwa ndani. Nyumba hiyo ipo eneo la Kokoto, mbele kidogo ya Mbagara Rangi Tatu karibu na Shule ya St. Marys .Alinikabidhi kwa hiyari nikiwa kama mshiriki wa kazi zake ili niweze kuishi pamoja na familia yangu. Kutoka tarehe niliyotaja hapo juu mpaka sasa mimi na familia yangu ya watu watano tumekuwa tukiishi nje hivyo kujikuta tukiishi kwa taabu sana . Uamuzi wa kuivunja nyumba hiyo ulitokana na mgogoro wa kikazi akinituhumu kwamba nimeacha kazi kwake kimyakimya jambo ambalo si kweli kwani hadi kufikia Januari 20 ,January 2015 bado nilitambulika na bodi ya Uhariri kama Mwandishi wa habari Mwandamizi. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, unyanyasaji pamoja na matumizi mabaya ya madaraka ambavyo amekuwa akitumia Mh. Diwani Mbwana. Pia ni ukatili mkubwa dhidi ya wafanyakazi pamoja na kielelezo cha jinsi waandishi wa habari hapa nchini tusivyo thaminiwa. Ninaiomba Serikali ,na wadau kunisaidia katika kipindi hiki kigumu kwani hivi sasa hali ni mbaya hasa upande wa familia yangu kwani nina watoto wadogo wakiwemo wa miaka 10,5 na 2 ambao kwa takriban siku tatu sasa naishi nao nje. nikiendelea kufuatilia taratibu za haki kuchukua mkondo wake. Aidha tunaishi kwa hofu kutokana na Diwani huyo kunipa tishio la mdomo kwamba ataniua tu. Mh. Diwani alitamka hayo tukiwa katika kikao cha usuluhishi katika ofisi za Serikali ya Mtaa Kimbangulile tar 17 jan 2015 ambapo na mimi niliripoti siku hiyo hiyo katika kituo cha Polisi Kizuiani, Temeke, na kweli alifika tar 18,jan 2015 na kujaribu kufanikisha jaribio la kuua kwa kuvunja nyumba wakati mimi na familia tukiwa ndani . Nalishukuru Jeshi la Polisi Temeke ambalo lilisimama imara kuinusuru familia yangu ambayo ilikuwa ndani wakati paa la nyumba hiyo likivunjwa huku vijana walioamrishwa na diwani huyo wakiwemo watoto wake wakipora mali zangu na kutoweka, vikiwemo vitendea kazi vyangu vya uandishi wa habari. (Jinsi ya kufika eneo la tukio ni Barabara ya Kilwa kituo Mbagala Kokoto katika kituo cha Mafuta cha Camell. ) Kwa maelezo zaidi 0654 58 67 88 CHRISTOPHER LISSA

No comments:

Post a Comment