Balozi
 wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akitoa nasaha zake kwa 
Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na 
Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini 
Oman,kushoto kwake ni Naibu Balozi wake Bw.Juma Othman.
Baadhi
 ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya 
Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini 
Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali
 Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
Baadhi
 ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya 
Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini 
Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali
 Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
 Mkuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya 
Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika mjini Mascut, 
nchini Oman Bi Khadija Batashy akitoa shukran zake kwa niaba ya wenzake 
baada ya kupewa nasaha na Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed 
Saleh wa katikati, kulia kwake ni Naibu Balozi Bw.Juma Othman  
Balozi
 wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya 
Pamoja na Wakuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi 
mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la
 Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman kulia ni Masha Hussein na kushoto 
ni Khadija Batashy. Picha na Faki Mjaka.
Balozi
 wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya 
Pamoja na Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa 
ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini 
Mascut, nchini Oman mara baada ya kuwapa nasaha zake. Picha zote na Faki
 Mjaka.
 Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na 
Mwandishi wa Chanel Ten Said Makala Ofisini kwake alipowaita kwa lengo 
la kuwapa nasaha Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya 
Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini 
Mascut, nchini Oman. Picha na Faki Mjaka. 
2
 Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima kushoto
 akimkaribisha  Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia
 kutoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa
 ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini 
Mascut, nchini Oman. Katikati ni Mkuu wa Msafara wa Watanzania hao Bi 
Khadija Batashy.
………………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar, akiwa Mascut-Oman 22/01/2015
 
Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho Kimataifa ya Sanaa, 
Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea nchini Oman wametakiwa kuitumia vyema
 fursa ya kimataifa walioipata kwa kufuata vyema Miongozo waliyopewa ili
 ziara yao iweze kuleta Tija.
Miongozo hiyo ni pamoja na Mashirikiano miongoni mwao,kujituma 
kwa bidii na kutumia lugha nzuri katika Maonesho hayo kwa kuzingatia 
kuwa Wananchi wengi wa Omani wanaelewa vyema Lugha ya Kiswahili.
Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Ali 
Ahmed Saleh wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa 
Maonesho hayo Ofisini kwake Mascut nchini Oman.
Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na Mahusino mema na 
Oman hivyo Washiriki hao wanapaswa wafanye kazi zao kwa bidii na 
kuzingatia kanuni na Maadili ya Oman.
Balozi Saleh ameongeza kuwa kufuata kanuni na sheria za Oman 
kutawafanya Wajasiriamali hao wa Tanzania kufanyakazi zao kwa utulivu 
bila ya kupata usumbufu jambo ambalo litazidi kuimarisha mahusiano mema 
kati ya Tanzania na Oman.
Amebainisha kuwa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyoifanya mwaka jana nchini humo imezidi 
kuyaweka pazuri mahusiano na kwamba Washiriki hao wanapaswa wayatunze na
 kuyalinda.
“Ndugu zangu Tanzania ina nafasi ya kipekee nchi 
Oman,tunaheshimiwa sana kuliko nchi yoyote hasa baada ya ziara ya Rais 
Kikwete, naomba Mahusiano haya muyaendeleze kwa kufanya kazi zenu kwa 
bidii na kuchunga maneno yenu maana hawa Waoman wanakijua vyema 
Kiswahili Mkiwasema Wanafahamu” Alinasihi Balozi Saleh.
Ameongeza kuwa Raia wa Oman wanautamaduni wa Kumsifu na 
Kumtukuza Mfalme wao Sultan Qabus kwa mengi mazuri aliyowafanyia hivyo 
Watanzania hao wanapaswa kulifahamu hilo na kulichukulia Tahadhari.
Balozi Saleh amesema Mashirikiano miongoni mwao ni Jambo muhimu 
na kwamba wote wamekuja kwa Niaba ya Jamhuri ya Tanzania na Sio Bara au 
Visiwani.
“Kitu kingine Mufahamu kuwa hapa Tunaiwakilisha Tanzania kwa 
hiyo Uzanzibari na Ubara usiwepo maana mukiupa nafasi 
utamusumbua,Tusimameni katika Jina moja tu la Utanzania ambalo ndio 
uwakilishi wetu kimataifa” Alisema Balozi.
Aidha ametoa Wito kwa Wajasiriamali ambao hawakupata fursa ya 
kushiriki Maonesho hayo kutokata tama na kuamini kuwa ipo siku nao 
watapata nafasi ya kushiriki Maonesho ya kimataifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki 
Maonesho hayo Bi Khadija Batashy alimshukuru Balozi Saleh na Wasaidizi 
wake kwa Mapokezi mazuri na Nasaha alizozitoa.
Aidha Bi Khadija alimuahidi Balozi huyo kuzifanyia kazi nasaha 
hizo ikiwemo kujituma, kuzidisha mashirikiano na kutumia lugha nzuri ili
 kuwavutia wateja katika Maonesho hayo.
Awali Mkuu wa Utawala katika Ofisi ya Ubalozi Bw. Abdallah 
Kilima wakati akimkaribisha Balozi aliishukuru nchi ya Mascut kwa kuzidi
 kuongeza njanja za kuimarisha mashirikiano ikiwa ni pamoja na Mwaliko 
wa Maonesho hayo.
Kilima aliwataka Washiriki hao kuwa kitu kimoja na kusaidiana 
kwa hali na mali jambo ambalo litaipatia sifa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania.
Maonesho hayo ya muda wa mwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na 
Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila 
ifikapo saa 10 za jioni na kufungwa saa 04 usiku kwa majira ya nchi ya 
Omani ambapo Washiriki huonesha bidhaa za nchi zao na Watu kunua bidhaa 
hizo.
No comments:
Post a Comment