Imebainika kuwa bendi maarufu ya 
muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni 
almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza na mwanamuziki 
Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja,bendi hiyo imejikuta ipo katika 
hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa kutumbuiza maomyesho 
zaidi katika msimu ujao wa joto.
Watayarishaji wa maonyesho makub
wa ya nje barani Ulaya 
wanashinikizwa na washabiki wao lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa
 Band kutokana na mdundo wao Bongo dansi,maporota hao baada kuwekwa roho
 juu na washabiki wao nao wamedhamiria kuwapambanisha washabiki hao na 
bendi hiyo yenye makao yake nchini Ujerumani,habari za uhakika zimetonya
 kuwa bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na 
Austria na maonyesho mengine katika msimu wa joto. 
Habari zimetonya kuwa hali hiyo 
inatokana na tabia za washabiki kushinikiza bendi ya Ngoma Africa  
kuwepo katika ratiba ya  mzunguko wa maonyesho makubwa pamoja na  
wanamuziki hao kukosa muda wa kupumzika.
Hata hivyo  inasemekana kamanda 
Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu ratiba 
hiyo ngumu na kuwaburudisha washabiki wao waliodata akili na jinamizi la
 muziki wa dansi wa bongo kule barani ulaya.Ffu-Ughaibuni pia wanasikika
 online at www.ngoma-africa.com

No comments:
Post a Comment