![]()  | |
| Hali wakati wa makabiliano kati ya waasi na walinzi katika ikulu ya Rais mjini Sanaa | 
![]()  | 
| Waasi wa Houthis | 
Makabiliano makali yametokea kati ya
 waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya usalama katika ikulu ya Rais 
ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu ya Rais.
Walioshuhudia
 makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama 
kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.
Awali, Rais Abd 
Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku
 moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya 
waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu
Makubaliano yalifikiwa lakini waasi wa Houthis waliendelea kuzingira ikulu ya Rais na makao ya waziri mkuu.
Kiongozi
 wa waasi hao anatarajiwa kutoa hotuba baadaye leo wakati baraza la 
usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kwa mkutano wa dharura kujadili 
hali nchini Yemen.
Kanali Saleh al-Jamalani, ambaye ni mkuu wa 
kikosi cha ulinzi wa ikulu ya Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, ameambia 
sjirika la habari la AP kwamba waasi haowalivamia ikulu nyakti za 
mchana.
Rais Hadi inaarufiwa hakuwa katika makao hayo wakati waasi walioivamia ikulu. 


No comments:
Post a Comment