Hivi
 Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. 
Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea
 katika uchaguzi Mkuu wa nchi.
Hivi
 sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23
 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na
 vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na 
kushiriki shughuli za chama.
Mojawapo
 ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki 
shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro. 
Mojawapo
 ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina
 ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na 
kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na 
kanuni za chama.
Hivyo
 natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa 
vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao 
kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa 
jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.


No comments:
Post a Comment