Katibu
 Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mti wa viungo aina ya 
Mdalasini wakati akipata maelezo kutoka kwa Othman Mohamed  mwenyekiti 
wa kikundi Kinachoendesha shamba la Spice Solution Farm lililopo 
Mwakaje  jimbo la Mfenesini Zanzibar  wakati aliposhiriki pia shughuli 
za upandaji wa miti katika shamba hilo, Katika ziara hiyo ambayo ni ya 
kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka
 2010 Kinana Anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la Spice Solution Farm Mwakaje Mfenesini. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia pilipili zilizolimwa katika shamba hilo huku akipata maelezo.  
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia viongo mbalimbali vilivyosagwa na kusindikwa tayari kwa kuuza kwa wateja. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
 kazi ya kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Mbuzini jimbo la 
Mfenesini huku akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini 
Magharibi Ndugu Yusuf Mohamed Yusuf. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Mama Khadija Issa Kibwana mara baada ya kuzindua mradi wa maji Mbuzini jimbo la Mfenesini.
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia
 bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi cha akina mama 
wajasiriamali cha Mshikamano Daima Kilichopo Mtopepo jimbo la Mtoni 
mjini Zanzibar. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. Shamsi Vuai Nahodha  wakishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Bububu. 
Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. Shamsi Vuai Nahodha  kushoto akiteta jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kwenye ofisi ya CCM tawi la Bububu. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya  wilaya ya Mfenesini. 
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Yusuf Mohamed Yusuf akizungumza katika mkutano huo wa ndani. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Mh. Masauni Yusuf Masauni. 
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano wa ndani 
Balozi
 Ali Karume akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara 
uliofanyika kwenye viwanja vya Geji jimbo la Mtoni mjini Zanzibar. 
Baadhi ya wananchi na wana CCM wakiwa katika mkutano huo. 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Geji Mtoni mjini Zanzibar. 
Naibu
 Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika 
mkutano huo amewataka wazanzibari kupiga kura ya ndiyo ifikapo aprili 30
 mwaka huu ili kuipitisha katiba mpya iliyopendekezwa. 
Baadhi
 ya wanaCCM wakinyoosha mikono yao juu kukubali kupiga kura ya ndiyo 
katiba mpya iliyopendekezwa ifikapo Aprili 30 mwaka huu. 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment