TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 19, 2015

Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya Iringa vijijini asema vijana wanawajibika kuchagua kiongozi wanayemtaka

HAFSA MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya iringa vijijini mkoani Iringa
HAFSA MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya iringa vijijini
mkoani akiapiwa kuwa mkuu wa wilaya pangani
HAFSA MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya iringa vijijini mkoani akisimikwa kuwa kamanda wa vijana.

Na: Fredy Mgumda,
Iringa, HAFSA MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya Iringa vijijini mkoani hapa ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya pangani Tanga amesema kuwa vijana wanawajibu kwa kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa manufaa ya jamii katika maendelo.
 
Wito umetolewa kwa Vijana mkoani iringa na Tanzania kwa ujumla
kujiandikisha katika dafutari la kudumu ili waweze kupata
vitambulisho vya kudumu pamoja na kujitokeza kupiga kula katika
katiba iliyopendekezwa.
 
amewataka wanawake kuondoa woga na kuuvaa ujasiri na kuwa na ushirikiano katika kugombea uongozi katika sekta mbalimbali kwani nafasi hizo hazibagui jinsia.
 
Aidha ametoa wito kwa wanchi na viongozi wa serikali kudumisha amani na pia kuliombea taifa kupata viongozi walio bora katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
 
Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema HAFSA MTASIWA
 
MTASIWA ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au
kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi
wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na
ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.
 
Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema HAFSA MTASIWA
 
Lakini HAFSA MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya iringa vijijini mkoani iringa amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
 
MTASIWA ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo
yasiyokuwepo.
 
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
 
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
 
Mbali na hayo MTASIWA amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
 
Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wamhaki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.

No comments:

Post a Comment