Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mbozi Bw. Elisey Ngowi akifungu 
semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya 
Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo 
hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni 
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi 
Ester Riwa na kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Vijana
 wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya wakisikiliza kwa makini mafunzo 
yaliyokua yakitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, 
Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari,
 Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa 
wa Mbeya.
Mwezeshaji
 kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa 
kulia akifafanua jambo walipotembelea mradi wa kikundi cha vijana cha 
Miranaco wanaomiliki duka la madawa muhimu katika Wilaya ya Mbozi Mkoa 
wa Mbeya. Kushoto ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa,
 wapili kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean 
Masele na wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Miranaco Bw. John 
Maige.
(Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)
…………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya
Tarehe 22/01/2015
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imeshauriwa kupeleka vijana wa 
wilaya hiyo katika Vituo vya Vijana kupata mafunzo mbalimbali ili kuweza
 kupata mbinu mbadala za kiujasiriamali.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Bw. 
Laurean Masele wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi 
na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi 
Mkoa wa Mbeya.
Bw. Masele amesema kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na 
Michezo inasimamia Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya kinachotoa mafunzo ya 
ujasiriamali katika fani za Kilimo na Ufugaji, Kituo cha Vijana cha 
Ilonga Morogoro kinachotoa mafunzo katika fani ya teknolojia ya habari 
na mawasiliano na Kituo cha Vijana cha Marangu Moshi kinachotoa mafunzo 
ya uthubutu/ujasiri kwa vijana.
Aidha Bw. Masele amesema kuwa moto uliowashwa na Wizara ya 
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhamasisha vijana mbinu za 
kiujasiriamali unalenga kuwajengea vijana ujasiri wa kuthubutu na 
kufikia malengo waliyojiwekea.
Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo Kaimu Mkurugenzi 
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Elisey Ngowi amewataka 
vijana kuzingatia elimu inayotolewa na kuifanyia kazi kwani vijana bado 
wanauwezo mkubwa wa kufikiri hivyo kutumia akili nyingi na nguvu nyingi 
kufanya mambo mbalimbali kwa maendeleo ya Wilaya hiyo.
Kwa upande wake kijana Yohana Chaula kutoka kikundi cha Bodoboda
 B. Mloo Wilaya ya Mbozi amesema kuwa kundi la vijana wasiokua na ajira 
kwa sasa linazidi kuongezeka hivyo kuiomba Wizara inayosimamia masuala 
ya Vijana kuongeza fungu katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili vijana 
wote nchini waweze kunufaika na Mfuko huo.
Naye mwakakikundi wa kikundi cha Umoja wa Vijana Wilaya ya Mbozi
 Bw. Chemli Ndema ameushukuru ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo kufika Wilaya ya Mbozi na kutoa elimu ya ujuzi kwa 
vijana kwani elimu aliyoipata katika semina hiyo imemtoa katika giza 
nene na kukiri kuwa atakuwa chachu ya maendeleo na kiongozi bora katika 
jamii. 
No comments:
Post a Comment