Waziri
 wa maji Jumanne Maghembe wa kwanza kulia akizungumza na wakandarasi 
wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati
 alipotembelea tembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji 
Safi na maji Taka (DAWASA),  kwalengo la kupata tathimini ya mradi huo 
ulipofikia sasa. 
Waziri
 wa Maji Jumanne Maghembe wapili kulia akioneshwa mchoro wa mradi wa 
bomba la maji  mlandizi kimara linalopitia makongo juu na Mhandisi wa 
Mradi huo, Bw Severin Mkendala jinsi mabomba  mradi wa mlandizi kimara 
yalipopita .
Waziri
 wa maji Jumanne Mghembe wa pili kulia akiwa ameongozana na meneja mradi
 Pintu Dutta watatu kulia wakati akikagua maendeleo ya mradi wa kituo 
cha kusafisha maji cha ruvu juu .
Mashine
 aina ya Catterpilar la kampuni ya Megha Enginearing Infastructure 
Limited, likiwa linasafisha eneo ambalo linatakiwa kulazwa mabomba ya 
yanayotoka Mlandizi Kimara kwenda Ruvu JUU. 
Kushoto
 ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure 
Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Waziri wa Maji 
Jumanne Maghembe,aliyekuwa katika ziara  ya kutembelea miradi  
inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka. 
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara hiyo.
 
Wafanyakazi wa kampuni ya WABAG Constraction wakiendela na ujenzi wa wa kituo cha kuasfisha maji cha ruvu juu .
…………………………………………………………………………………….
WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe 
ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limitedi
 anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi 
huo na kupeleka ripoti ya maradi,mamlka ya maji safi na maji taka 
(Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi.
Alitoa agizo hilo Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati akikagua 
miradi minne ya Dawasco,yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini 
kufikisha Jijini Dar es Salaam.
Alisema,mpaka sasa mkandarasi alitakiwa aweamelaza kilomita 20,lakini chakushangaza mkandarasi huyo amelaza kilomita 12,tu.
Maghembe alisema utendaji kazi wa mkandarasi huyo ni mbovu na 
nimewaagiza wabadilike na nitakuja kuwatembelea baada ya siku 90,na kama
 hakutakuwa na maendeleo itabidi tuwafukuze.
“tumempatia mkandarasio huyu kiasi cha dola za kimarikani 
59,ambao nisawa na bilioni 96 za kitanzani fedha hizi watanzania 
watazilipa hivyo ni vema mkandarasi huyu afanye kazi iliyomleta,”alisema
 Maghembe
Kwaupande wa maradi wa Ruvu juu wa kusafisha maji Waziri 
Maghembe aliridhika na utendaji kazi wa mkandarasi anayejenga mradi huo 
na kumtaka amalizie kufunga pampu mpya ili mgao wa maji upungue Dar es 
Salaam.
Aidha alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa 
kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa siku ya
 Alhamisi.
No comments:
Post a Comment