TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 23, 2015

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti_______________________
Na demasho.com
 Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
imefanya tahimini ya elimu ya na matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi
mwaka 2014 katika ukumbi wa EMAU Peremiho.
Katika tathimini hiyo mkuu wawilaya ya Songea
Joseph Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa, Watendaji wa kata  na Watendaji wa Vijiji kuwapa elimu wazazi
juu ya umuhimu wa kuchangia chakula cha kutosheleza muhula wa masomo
ili kusaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo
Kwani kufanya hivo kutasaidia wanafunzi kujifunza muda wote wawapo shuleni na kujenga ushirikiano baina yao wanapokuwa pamoja na hali hiyo iatainua kiwango cha ufaulu” alisema Mkirikiti.
Hata hivyo Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa,
Watendaji wa kata  na Watendaji kuacha
kusingizia wanasiasa kuwa wamezuia suala la kuchangia chakula
Tabia ya kuwasingizia wanasiasa kuwa wamezua kuchangia chakula mashuleni muache sio kila kitu kusingizia wanasiasa hivi ni kiongozi gani asiependa maendereo ?, maana saiz kila kitu wanasiasa wamezuia hasa kipindi hiki tunachoenda cha uchaguzi utasikia wanasiasa wamezuia ukiona mwanasiasa anazuia basi huyo ni SHIDAAA Alisema Mkirikiti.
Naye Kaimu Afisa elimu wilya Bw. Tanu Kameka ameomba baada ya Tathimini hiyo wakutane na waratibu wakata, wazazi , walimu pamoja na watendaje ili uongezwe muda wa ziada wa ufundishaji ili kuweza kuleta mwamko wa elimu katika halmashauri hiyo ya Songea vijijini na kuleta ufaulu mzuri.
 “ Miaka yote tumekuwa tukifanya hivo na ndiyo maana
tukawa tunaongoza katika matokeo , ila kwa mwaka jana hatukuweza kusimamia hili swala la muda wa ziada ndiyo maana tumeshuka ila kwa mwaka huu tunalirudisha swala la muda wa ziada hivyo tutafanya vizuri katika matokeo Alisema Bw.
Kameka.

No comments:

Post a Comment