TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 21, 2015

KUTANO MKUU WA BARAZA LA WATOTO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUFANYIKA DODOMA KUANZIA TAREHE 20 – 21 JANUARI, 2015

…………………………………………………………………………………
Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni chombo cha kuwashirikisha watoto katika maamuzi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Baraza la Watoto lilianzishwa mwaka 2002 likiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa watoto katika ngazi mbalimbali za jamii kama mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (CRC) ulivyoeleza ambapo Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa mataifa unapaswa kuutekeleza. kila baada ya miaka 2 Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanya mabadiliko ya uongozi katika kuliendesha Baraza la watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia na mwaka huu uchaguzi utafanyika tarehe 21 Januari 2015 baada ya ule wa mwaka 2013. Wizara Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto hufanya uratibu na kusimamia uanzishwaji na uendeleshaji wa Baraza hili na mengine yaliyopo katika mikoa yetu. serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuboresha ushiriki huo wa mtoto kwa kuchukua hatua mbalimbali kama ifuatavyo. · Kuandaa katiba ya Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania · Kuandaa mwongozo wa uundwaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi za Taifa,mikoa,wilaya,kata na vijiji/mitaa. · Kuandaa na kusambaza kielekezi cha ushiriki wa mtoto · Kuandaa mpango kazi wa Taifa wa ushiriki wa mtoto · Kuwashirikisha watoto katika maamuzi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa – km kutoa maoni katika utengenezaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maandalizi ya sera ya mtoto ya afrika mashariki ambapo wawakilishi wa watoto nchini walishiriki.

No comments:

Post a Comment