Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, 
Mathias Chikawe (kulia-meza kuu) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la 
Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya kiutumishi na kiutendaji 
wa askari katika Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani
 ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa 
Wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya 
Mambo ya Ndani ya Nchi.
 PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimuapisha Afisa wa
 Jeshi la Magereza, Elmas Linus Mgimwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya 
Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi
 na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo 
jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Chikawe ni Naibu Waziri wa 
Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na katikati ni Katibu Mkuu 
wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya 
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa hati ya kiapo
 Afisa Utumishi wa wizara hiyo, Ernest Maalugu kuwa Mjumbe wa 
Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia 
masuala ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi
 wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo
 ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Katibu Mkuu wa 
Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo 
ya Ndani ya Nchi.

No comments:
Post a Comment