Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius 
Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa tayari kutiliana saini 
mkataba wa makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga.
 Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa 
Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia.Fedha
 hizo zimetoka BADEA.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.    Servacius 
Likwelile akitia saini makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya 
Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye 
ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa
 Saudia. Aliyeko kulia ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka 
Wizara ya Fedha.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.   Servacius 
Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na 
Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakibadilishana 
mikataba hiyo baada ya kutiliana saini.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.   Servacius 
Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na 
Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakiionyesha 
mikataba hiyo kwa waliohudhuria sherehe hiyo baada ya kutiliana saini.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius 
Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na 
Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakicheka na 
kugonga kwa furaha baada ya kukamilisha shughuli ya kusainiana mkataba 
wa kuweka mradi wa maji wilayani Same na Mwanga
Picha zote na Ingiahedi Mduma-Wizara ya Fedha tukiwa Washington DC.
……………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na 
Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, mchana wa leo 
ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa kuanzisha Mradi wa Maji 
katika Wilaya ya Same na Mwanga. Dr. Likwelile alisaini Mkataba huo kwa 
niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Kiarabu
 ya Maendeleo ya uchumi ya Afrika . Aliye wakilisha Benki hiyo ni Eng. 
Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi 
Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia. 
Aidha katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile 
alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa Serikali ya Tanzania inatambua 
kuwa BADEA imetoa Dola za Kimarekani milioni 12.0 sawa na shilingi 
Bilioni 20.1 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika 
Wilaya ya Same na Mwanga. Hivyo inatoa shukrani zake za dhati kwa BADEA 
kwa kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania. 
“Msaada huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la
 maji katika wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi BADEA 
unaunga mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika masuala ya 
kijamii na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo tunaomba 
muendelee kutusaidia”. Alisema Dr. Likwelile. 
Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa, kama 
anavyofahamu gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani
 million 110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine
 kama mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na 
Serikali kuchangia fedha kusaidia mradi huu. Kwa hili sina wasiwasi nalo
 kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana na ninaujasiri kuwa 
jitihada zako zitafanikiwa.
“Mradi huu wa maji wq wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia
 kuwepo kwa maji kwenye jamii mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo.” 
Aliongeza Dr.Likwelile.
Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika :
(i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa.
(ii) Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya 
kwa jamii nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi.
(iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka.
“Mafanikio ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa 
uchumi wa jamii na maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga”. 
Alisema Likwelile.
Dr. Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa“Tanzania na Saudia ni 
marafiki wa muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha 
kila kitu kinaenda sawa”. 
Hali ya hewa ya mjini Washington Dc. ni mvua za vipindi na baridi kiasi.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji – Wizara ya Fedha
Washington D.C
11/10/2014
No comments:
Post a Comment