Mwenyekiti
 wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda akizungumza 
na wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke kamati hiyo ilitofanya ziara ya 
kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa 
Maendeleo ya Vijana katika manispaa hiyo jana jijini Dar es Salaam. 
Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Maabad S. Hoja na 
wamwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo  
Mwenyekiti
 wa Temeke Vijana Saccoss Bw. Swaka Abbas akisoma taarifa fupi ya 
maendeleo ya Saccoss yao mbele ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii 
(hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilifanya ziara 
ya kutembelea niradi ya inayoendeshwa na Vijana kupitia Vikundi 
vilivyopata mkopo kutoka katika Mfuiko wa Maendeleo ya Vijana 
Mstahiki
 Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Maabad S. Hoja akifafanua jambo wakati 
wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipofanya
 ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyopata mkopo kutoka Wizara 
ya Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Bw. P. Kagimbo, 
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia 
(MB) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad 
Mtanda
Baadhi
 ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo 
wakifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa
 Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa
 Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani) 
wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa
 hiyo jana.  
Kushoto
 ni mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Dkt. Maua Daftari 
akifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa 
Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa 
Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani) 
jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya 
Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Na Concilia Niyibitanga
Vijana wanatakiwa kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii kama njia pekee ya kujikwamua na umasikini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya 
Jamii, Mhe. Said Mtanda (Mb.) jana wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua
 miradi inayoendeshwa na vikundi vya vijana katika Halmashauri ya 
Manispaa ya Temeke vilivyopata mikopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo 
ya Vijana unaoratibiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na 
Michezo.
Mhe. Mtanda alisema kuwa ajira za maofisini haziwezi kutosheleza
 kila kijana kutokana na ukweli huo ni wakati wa vijana kupambana na 
hiyo changamoto kwa njia ya kujiajiri kwa kubuni miradi ya 
kuwatengenezea kipato hali itakayowakwamua katika umaskini.
“vijana msiogope kuthubutu siyo lazima kuanza na mradi mkubwa 
anza na huo huo mdogo ipo siku utakuwa mradi mkubwa hata mbuyu ulianza 
kama mchicha”. Alisema Mhe. Mtanda.
Miradi iliyokaguliwa na Kamati hiyo ni pamoja na mradi wa kilimo
 cha matikitimaji, mapesheni na ufugaji kuku unaoendeshwa na Kikundi cha
 Vijana kijulikanacho kama Sokoine Youth Development kilichopo kata ya 
Somangila, Kigamboni.
Kikundi kingine kilichokaguliwa ni kikundi cha vijana 
waliohitimu na walioko vyuo vikuu kijulikanacho kama African Legends 
kilichopo Kigamboni; kikundi hiki kinachojishughulisha na mgahawa pamoja
 na maswala ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Aidha, Kamati hiyo ilikagua kikundi cha Vijana cha Waungwana 
Youth Family kinachojishughulisha na kazi za saluni pamoja na muziki; 
kikundi hiki kiko katika kata ya Sandali.
Mhe. Mtanda aliwakumbusha vijana umuhimu wa kujiunga katika 
vikundi vya vijana ili watambulike na wajiunge katika SACCOS za vijana 
katika Halmashauri wazoishi ili iwe rahisi kukopa katika Mfuko wa 
Maendeleo ya Vijana.
Naye Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. 
Juma Nkamia (Mb.) alisema kuwa Wizara imejipanga kuwawezesha vijana 
kujikwamua kiuchumi na imekuwa ikitoa elimu ya ujasiriamali na stadi za 
maisha zoezi ambalo ni endelevu kwani hadi sasa wataalamu wanazunguka 
katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kazi hiyo.
Mhe. Nkamia alisema kuwa Wizara itaendelea kuwezesha vikundi vya
 vijana ambavyo tayari vina miradi ili iweze kukua zaidi na kuwa miradi 
mikubwa yenye uwezo wa kutengeneza ajira kwa vijana wengine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa SACCOS ya Vijana ya Temeke, Bw 
Swaka Abbas ambapo ndiko mikopo ya vikundi hivyo ilikopitishiwa 
aliishukuru Kamati hiyo kwa kuwatembelea na kuwatia moyo. Pia 
aliishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na 
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa ushirikiano wanaoupata katika kazi
 zao za kutokomeza umaskini.
No comments:
Post a Comment