Mahmoud Ahmad Dar es Salaam                                   
JAMII imeshauriwa kuendelea 
kutoa taarifa kwa jeshi la polisi dhidi ya watu wanaomiliki silaha 
kinyume cha sheria kwani wasababisha uvunjifu wa amani kwa raia na mali 
zao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa 
Wilaya ya Temeke Bi.Sophia Mjema,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika 
sherehe ya utoaji sifa na zawadi kwa maofisa wakaguzi na askari 107 wa 
vyeo mbalimbali,kutokana na umahili wao wa kupambana na uhalifu kwa 
Kanda Maalum ya Dar Es Salaam.
Bi.mjema alisema kazi ya polisi 
ni kulinda usalama wa raia na kuwakamata wahalifu ambao ndio chanzo cha 
uvufu wa amani,hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana na poli kwa ajili 
ya usalama wao na  taifa kwa ujumla.
Aidha aliwataka wale wanaomiliki
 silaha kihalali wazitumie kwa kufuata sheria na si vinginevyo,pia 
waache tabia ya kuwatishia raia wenzao kwa kuwa wanaumiliki halali,na 
endapo watabainika na tabia hizo watanyang’anywa silaha zao mara moja.
“wapo baadhi ya watu huko 
mitaani wanamiliki silaha kinyume na taratibu za kisheria,msiwafumbie 
macho wala kuwaonea muhali,hata kama ni ndugu yako tunaomba mtoe taarifa
 kwa jeshila polisi litawashughulikia,pia kuna baadhi ya wale waomiliki 
kihalali silaha hizo lakini wanazitumia kinyume cha sheria kwa kufanya 
uporaji na kuwatishia raia mitaani,suala ambalo ni la hatari na haliwezi
 kuvumiliwa likiendelea,hivyo hakuna budi kuwafichua ili hatua zaidi 
zichukuliwe dhidi yao”
Bi.Mjema amewataka wajisalimishe
 haraka wale wote wanaomiliki silaha pasipo kufuata sheria,kabla jeshi 
la polisi halijaanza msako mkali,kwani atakayekutwa na silaha 
atafikishwa mbele ya dola kujibu mashtaka ya kukadi na kusababisha 
uvunjifu wa sheria.
Kwa upande wake Kamishna wa 
Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova,ameliomba jeshi la polisi 
kufanya kazi kwa weledi mpana zaidi,kwa kufuata misingi na taratibu 
zilizowekwa,katika kulinda na kufichua wahalifu,ili nchi iendelee kuwa 
na amani ambayo ndio tunu a taifa letu.
“Tunataka nchi hii iendelee kuwa
 kisiwa cha amani na hatukubali kabisa mtu yeyote alete chokochoko za 
aina yeyote awe chanzo cha kutoweka kwa amani yetu ambayo ni zawadi 
kutoka kwa mwenyezi mungu,kupitia waasisi wa yaifa hili ambao 
walituletea uhuru,hivyo nyinyi kama askari mhakikishe mnawakamata na 
kuwatia hatiani wale wote watakaothubutu kuhatrisha amani ya 
nchi”.alisema Bi. Njema
Naye  Mwenyekiti Wa Kamati Ya 
Ulinzi Na Usalama ambaye pia ni sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh 
Alhad Musa Salum,alizungumzia suala la baadhi ya wanasiasa ambao 
wamekuwa wakijipitisha katika nyumba za ibada kufanya kampeni kwa 
manufaa yao binafsi ili wananchi wawape kura,kamwe suala hilo 
halikubaliki na wanatakiwa kujiheshimu na kuacha tabia hiyo mara moja.
“Tayari tumejipanga kikamilifu 
kuhakikisha wanasiasa wanaheshimu nyumba za ibada,na kwamba siasa zao 
wazifanyie uraiani na sio misikitini wala makanisani,na wananchi 
wawakatae viongozi wanaotumia pesa kuomba kura na wasiwachague”.
Aidha ametoa wito kwa tume ya 
taifa ya uchaguzi (nec),ifanye kazi yake kwa uadilifu na kwa makini 
zaidi kwa kuweka utaratibu ambao ni mzuri kwa wapiga kura katika chaguzi
 zijazo za katiba na uchaguzi mkuu ujao,na kuachana na mambo ya 
ubabaishaji ambayo yamekuwa yakileta taflani.

No comments:
Post a Comment