Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni  ya Uwekezaji 
ya UTT, Migangala Simon.
Ofisa 
Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni  ya Uwekezaji ya UTT, Migangala Simon 
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es 
Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa uwekezaji katika soko la hisa kwa nchi
 zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki.
Dotto Mwaibale
KAMPUNI 
ya Uwekezaji ya UTT imesema ushirikiano wa uwekezaji katika soko la hisa
 wa nchi za jumiya ya Afrika Mashariki utaleta tija kwa nchi hizo.
Akizungumza
 Dar es Salaam leo Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Migangala 
Simon alisema uwepo wa ushirikiano utasaidia hata nchi moja ikiwa na 
matatizo iwe rahisi kusaidiana.
“Kwa 
mfano Tanzania sasa hivi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao unatarajia
 kufanyika Oktoba mwka huu inavyoelekea hivyo fedha nyingi zitatumika 
lakini kukiwepo na ushirikiano na umoja ni lazima nchi nyingine kusaidia
 kupitia soko la hisa,”alisema.
Alisema 
kampuni hiyo ina jumla ya mifuko mitano,kuna mfuko wa umoja,wekeza 
maisha, mfuko wa watoto,mfuko wa ukwasi na mfuko wa jikimu.
Simon alisema mifuko yote ina lengo la kusaidia wananchi wote walio katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Pia huwa
 tunawasaidia watoto katika maendeleo yao hapa nchini hususani elimu 
 watoto hao ni wale walio chini miaka 18,”alisema. 
Simon 
alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujiunga na kampuni hiyo na 
kuweka hisa zao ambapo watapata gawio kubwa kulingana na hisa 
walizoweka. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment