Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu 
wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili katika kijiji
 cha Kikobweni jimbo la Chaani mkoa wa Unguja Kaskazini  akiwa katika 
ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 
mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja  kuhimiza uhai wa 
Chama Cha Mapinduzi mahali ambapo kimelegalega na kuongeza nguvu mahali 
ambapo kinatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, Katika ziara hiyo Katibu 
Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi
 na Uenezi. 
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akielekea kwenye ukubi wa 
Mkorea mahali ambapo mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Unguja 
Kaskazini umefanyika. 
Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za kupanda 
migomba wakati alipokitembelea kikundi cha akina mama cha  Tuko Imara 
kinachojishughulisha na shughuli za kilimo cha Migomba, Mbogambona na 
Mananasi katika kijiji cha  Banda Maji. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai naye akishiriki kupanda migomba wakati  Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokitembelea kikundi hicho na 
kujionea shughuli zao za uzalishaji wa mazao ya kilimo.  
Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya kilimo cha 
mananasi kutoka kwa Bi Mayasa Abdallah Juma Mwenyekiti wa kikundi cha 
Tuko Imara wakati alipokitembelea kikundi hicho.  
Katibu
 Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za 
kusafisha visiki katika mradi uliobuniwa na wananchi wakisaidiwa na 
TASAF kwa ajili ya utengenezaji wa barabara inayounganisha kijiji cha 
Kijini kwa Shauri Pili kwenda katika kijiji cha Kirwa. 
 
Baadhi ya wananchi wakiondoka mara baada ya kufanya kazi ya kusafisha barabara hiyo kwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.  
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa nyumba ya madaktari katika kijiji cha Kijini Hospitali jimbo la Matemwe. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia
 mchezo wa sarakasi uliochezwa na vijana  wa Kijini Hospitali wakati 
alipotembelea ujenzi wa nyumba wa madaktari katika kijiji hicho 
Baadhi
 ya viongozi wa timu mbalimbali za jimbo la Nungwi wakiwa na jezi na 
mipira yao mara baada ya kukabidhiwa kwenye uwanja wa Tazari ambapo pia 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alishiriki katika ujenzi wa 
ukuta wa uwanja huo. 
Mwandishi
 wa habari kutoka kituo cha televisheni cha Star TV ambaye yuko katika 
ziara hiyo akishiriki kupiga Dufu katika kijiji cha Banda Maji.  
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa jimbo la Nungwi katika uwanja wa Skuli mjini Nungwi. 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo. 
 
Baadhi ya wanahabari ambao wako katika ziara ya  Katibu Mkuu huyo wakiwa kazini. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akitema cheche zake mjini Nungwi. 
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Skuli mjini Nungwi. 
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama wa chama hicho. 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwaaapisha wanachama wapya wa CCM kwenye uwanja wa Skuli mjini Nungwi.
No comments:
Post a Comment