
……………………………………………………………………………………………………………
Na Gladness Mushi-Ngurudoto Arusha
 Waandishi wa habari kutoka katika
 vyombo mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kuipelekwa nchini Sudan 
Kusini ili kujifunza athari za vita ambazo zimetokea katika nchi ya 
Sudani kusini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu 
mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,leo wakati 
akizungumza na waaandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini  baina 
ya vikundi vinavyogombana kutoka nchini Sudani.
Kinana amesema kuwa baada ya 
kuwekeana saini na makubaliano ya kuacha mapigano basi Nchi ya Tanzania 
itachukua jukumu la kupekeka waaandishi wa habari Sudani kwa malengo  ya
 kujifunza na kujionea athari za vita .
“Tunataka waandishi wetu wa habari kutoka Tanzania wapate  uelewa wa kutosha katika kuandika na kutangaza madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, Kinana aliahidi kuwa ni muhimu na atahakikisha anawapeleka waandishi wa habari  waitembelee Sudan Kusini,”alisema.
Kinana alifafanua kuwa yeye binafsi anaamini watakapokwenda kujionea kwa macho madhara ya vita wataweza kutumia vema kalamu zao kuelimisha watanzania madhara ya vita.
Chama Cha Mapinduzi (CCM)kiliombwa kufanya na kusimamia mazungumzo juu ya vita hiyo na ndivyo watakavyofanya pia kwa waandishi ili wapate somo.
Alisema mapigano hayo yamesababisha uchumi wa nchi hiyo kurudi nyuma,ukizingatia kuwa wao ni wazalishaji wakubwa wa ng’ombea na watatu katika nchi za Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambapo pia wana utajiri mkubwa wa mafuta.
alisema Sudan Kusini ilihangaika miaka zaidi ya 50 kutafuta uhuru wao, miaka miwili baada ya kujitenga kutoka Sudan Kaskazini, baada ya asilimia 90% kupiga kura ya kujitenga wakaanza vita ya kugombea madaraka, sasa kila familia imeathirika kutokana vita ndio wanasaka amani.
Mazungumzo ya kutafuta amani kwa nchi hiyo yalianza mapema Desemba 23 na 24 mwaka jana 2014 katika Hotel ya Ngurudoto, Wilayani Arumeru,Mkoan Arusha, huku zikiwakutanisha pande zote tatu zinazopigana kwa ajili ya kusaka madaraka.
Katika mazungumzo hayo mwenyekiti wa mazungumzo hayo ni Balozi Dk.
John Samwel Malecela, ambaye pia alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu awamu ya pili ya uongozi wa Rais Ally Hassan Mwinyi.
Mapigano hayo ya ndani ya chama cha SPLM katika nchi ya Sudani Kusini yanahusisha makundi matatu ambapo kila kundi linataka madaraka ya
kuongoza nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment