KAMATI  YA  BUNGE YA ARDHI, 
MALIASILI NA MAZINGIRA IMEAGIZA WIZARA YA  ARDHI NYUMBA NA MAKAZI PAMOJA
 NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ZIKAE  NA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI 
ULIYOPO KWENYE HIFADHI YA TAIFA YA SAADANI
MAAGIZO HAYO YA KAMATI 
 YAMETOLEWA LEO  JIJINI DAR ES SALAAM NA MWENYEKITI WA KAMATI  HIYO 
MBUNGE WA KAHAMA MHESHIMIWA JAMES LEMBELI.
 KABLA YA KAMATI KUTOA MAAGIZO 
KWA WIZARA HIZO,KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII DOKTA 
ADELHELM MERU AMEIELEZA KAMATI KWAMBA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
 TANZANIA ILITENGA ENEO HILO KUWA SEHEMU YA HIFADHI YA TAIFA YA SAADANI.
AMESEMA KATIBU HAPO AWALI ENEO 
HILO LILIKUWA NI SHAMBA LA MIFUGO LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 
AMBAPO NDANI YA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI ZOTE ZIKAKUBALIANA KUTENGA 
ENEO HILO KUWA HIFADHI YA AKIBA HADI MWAKA 2005 NDIPO ILIPOTANGAZWA 
RASMI KUWA HIFADHI KAMILI.
NAYE KATIBU MKUU WA WIZARA YA 
ARDHI BWANA ALPHAYOL HIDATA AMESEMA WIZARA YAKE HAPOAWALI HAIKUWA NA 
TAARIFA ZA KUWA ENEO HILO LIMETENGWA KWA AJILI YA HIFADHI NA NDIPO 
WAKAMMILIKISHA MWEKEZAJI KWA AJILI YA KILIMO CHA MIWA

No comments:
Post a Comment