Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo 
Mohamed Asenga Akifungua kikao cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki 
,kulia kwake ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya 
Sitalike Slivester Nswima na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Said Juma Maraba.
Wataalam wakifuatilia kwa umakini mjadala wa  kikao cha madiwani Halmashauri ya Nsimbo
(Picha na Kibada Ernest-Katavi)
……………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada –Katavi
Madiwani  wa  
Halmashauri ya Nsimbo   Wilaya ya Mlele  Mkoa wa   Katavi   wameshauriwa
 kupima Afya zao na hasa  maambukizi ya VVU  kabla ya kuchukua fomu za 
kugombea Udiwani kwenye Kata zao  ili waweze  waweze kuwa mfano kwa watu
 wanaowaongoza na kutambua afya zao   kama kweli watakuwa na nguvu za 
kutosha kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa kipindi cha kuwepo 
madarakani. 
Diwani  wa Kata 
ya Kapalala  Reward Sichone alitowa ushauri huo   kwenye kikao cha 
Baraza la Madiwani   Halmashauri ya Nsimbo  baada ya kuwasilishwa kwa 
 taarifa ya kamati ya kuthibiti ukimwi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa 
hiyo Diwani wa Kata ya Sitalike Silvester Nswima. 
 Diwani Sichone 
alieleza kuwa ni  vizuri kwa madiwani  hasa wa Halmashauri  ya wilaya ya
 Nsimbo wanao tarajiwa kumaliza muda wao mwaka huu wakaandaliwa 
utaratibu na Halmashauri  wa kupimwa maambukizi ya VVU kabla ya kumaliza
 muda wao wa uongozi mwaka huu ili waweze kuwa mfano kwa watu wao wanao 
waongoza.
 Alilieleza 
Baraza hilo la  madiwani kuwa  endapo  watapimwa afya zao  mapema  
itawafanya wajitathimini  kabla ya kuchukua fomu za kugombea  udiwani. 
 Sichone 
alisema  endapo diwani atapimwa na kukutwa anamatatizo kwenye  afya 
yake  itamsadia  kuona kama kweli atakuwa na uwezo wa nguvu za kufanya 
kazi za wananchi  kwenye eneo lake.   
 Alifafanulia 
kuwa haitakuwa vizuri kwa diwani ambaye atapimwa na kukutwa  na 
maambukizi ya VVU  halafu  achukue fomu za kugombea tena wakati anajua 
kuwa hana nguvu za kufanya kazi za wananchi wake   hivyo swala la 
madiwani kupima  afya zao ni jambo   la msingi sana
“Jamani mnacke 
lakini mambo haya ni muhimu sana katika jamii zetu hasa wananchi 
tunaowaongoza wakiona tunafanya namna hiyo wanakuwa na imani nasisi 
ingawa kupima siyo lazima ni hiari ya mtu “alisema Diwani Sichone. 
 Kwa upande 
 wake Mwenyekiti  wa Kamati ya kudhibiti  Ukimwi  wa Baraza  la 
Madiwani  Sylvester Nswima  ambae ni Diwani wa Kata ya Sitalike 
alipinga  ushauri huo wa Diwani Sichone
Nswima alieleza 
kuwa  swala la Madiwani  kupimwa afya zao kwa pamoja  haiwezekani kwani 
kupima ni  hiyari ya kila mtu na sio lazima,hivyo kila mtu atapima kwa 
muda wake na kwa hiari yake. 
Naye Mwenyekti 
wa  Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alisema   kitendo cha 
 madiwani kupima afya zao  kinaweza kuwa  ni mfano mzuri kwa watumishi  
na wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo kuona viongozi wao wakimwa afya 
  na kuwafanya nao wataiga mfano wa kupima mara kwa mara afya zao. 
 Aliwatoa 
wasiwasi kwa kusema kuwa “Madiwani tusihofu kupimwa   bali tuangalie 
utaratibu wa  kuwaita wataalamu waje watupime afya  ili tuwe mfano kwa 
watu wengine  kwenye Halmashauri yetu  na Mkoa wa Katavi kwa ujumla 
wake”alisema Mwenyekiti Mohamed Assenga. 
Katika taarifa 
ya utekelezaji wa shughuli za ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa 
hiariwalifanikiwa kupima watu 1221 kati ya wanaume 668 na  wanawake ni 
551 ambapo kati ya watu hao waliopima waliokutwa na maambukizi walikuwa 
watu 36 kwa Halmashauri ya Nsimbo.


No comments:
Post a Comment