TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 5, 2014

CHADEMA HAKINA MFUMO THABITI WA KIUONGOZI WA KUUNDA SERIKALI YA TANZANIA MWAKA 2015.


 
NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema anatamani kuona Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiingia Ikulu, ikibidi katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. 
Ndugai, amesema hatua hiyo inatokana na jinsi umma na taasisi zake vikiwamo vyombo vya habari, ‘vinavyokibeba’ chama pasipo hicho kutafakari kuhusu udhaifu wa Chadema.


Naibu Spika alisema, Chadema ni chama kinachoungwa mkono, lakini hakina mfumo thabiti wa kiuongozi unaoshawishi ama kukipa hadhi ya kuunda serikali.

“Lakini sasa watu wanakiona kama ndio mbadala kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitu amba

cho si kweli…ninatamani sana kuiona Chadema inaingia Ikulu ili watu wauone udhaifu huo na waandishi wataiandika vipi itakapokuwa madarakani,” alisema.

Ndugai alisema pamoja na azma hiyo inayolenga kuiaminisha jamii kwamba Chadema haina mfumo bora wa uongozi, CCM inabaki kuwa chama imara, lakini kikikabiliwa na changamoto mbalimbali.
 
Alisema, miongoni mwa changamoto hizo ni dalili za kuporomoka kwa umoja miongoni mwao, huku miongoni mwao wakielekea katika kuzitukuza pande za Muungano wanazotoka.


“Hata ndani ya Bunge wakati mwingine unaweza kuona mgawanyiko kwa wabunge wa CCM, lakini sasa bado kinaendelea kubaki kuwa chama tawala,” alisema.
 
Mbunge mmoja wa Chadema ambaye hata hivyo hakutaka jina lake kutajwa gazetini, aliungana na Ndugai, kwa nyakati tofauti, akisema chama hicho bado kina upungufu katika safu yake ya uongozi.
 
Kwa mujibu wa Mbunge huyo, uongozi wa Chadema bado unakabiliwa na changamoto nyingi kuanzia maadili binafsi, stadi na uwezo wa ki-uongozi katika kuchukua madaraka ya nchi.


“Tunakabiliwa na changamoto nyingi ambazo kwa Bahati mbaya, viongozi wetu hawapo tayari kutusikiliza sisi tulio ndani, matokeo yake ni kupunguza kasi ya ukuaji wake,” alisema.
 
Hata hivyo, Mbunge huyo alisema Chadema inahitaji kupata wabunge wengi katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mwakani, ili kukifanya kitime wajibu wa kujiimarisha katika ngazi za msingi.


Alisema uwepo wa wabunge wengi wa Chadema, kutasaidia kuchagiza kasi ya mabadiliko hasa ya kimfumo ikiwa ni njia ya kukifanya chama hicho kikidhi hitaji la kuunda serikali kwa miaka ijayo.
 
 

VITA DHIDI YA UFISADI.
 

Mbunge huyo aliikosoa Chadema kwa namna inavyoshiriki vita dhidi ya ufisadi, na kusema inawakwaza baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa kujiunga. 
Alisema ni kweli kwamba ufisadi hautakiwi kwa vile unakwamisha azma ya kufikia maendeleo endelevu na ustawi wa jamii, lakini nadharia inayoelekezwa kwa baadhi ya viongozi, pasipo kujali uadilifu wao na uwezo wa kiuongozi, unakifanya chama hicho kuwakosa ‘watu makini’ zaidi.
 
“Kuna watu wengi ambao wakijiunga Chadema, CCM itapasuka na kuwa mwanzo wa kuondoka madarakani, lakini wanashindwa kuja kwa sababu wameshatajwa na wengine wanaogopa kuhusishwa na ufisadi,” alisema.
 
 

CHADEMA YAMJIBU.
 

Hata hivyo, Chadema imemkosoa Ndugai na kusema kiongozi huyo ameonyesha udhaifu katika kuliongoza Bunge. 
“Ndugai ameonesha udhaifu kuliongoza Bunge na mara zote, udhaifu huo uliibuliwa na kuwekwa wazi na wabunge wa CHADEMA, hawezi kusema chama kina uwezo duni wa kiuongozi,” alisema Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene.
 
Makene, alisema kwa takribani miaka 10 sasa, Chadema kupitia viongozi na wabunge wake, imekuwa ikiilekeza serikali ya CCM (kwa niaba ya Umma), namna bora ya kuutumikia umma, ingawa (serikali hiyo) sio sikivu.
 
Alisema umma unakiunga mkono chama hicho kutokana na wanaona ubunifu, matumaini, haki, uwezo, ufahamu, umakini, uwajibikaji, utayari, maadili, misimamo na mawazo mbadala kwa ajili ya maslahi ya watanzania.
 
“Watanzania si wajinga kuamua kuchagua kwenda na Chadema, wameuona uongozi bora, sera endelevu, mikakati thabiti na oganaizesheni imara,” alisema.
 
Kuhusu ‘kubebwa’ na vyombo vya habari, Makene alisema hiyo ni hoja iliyokufa na kwamba ni dharau kwa wanahabari.

No comments:

Post a Comment