Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Video Productions
 imetoa tamko kwamba mwaka huu wamejipanga vizuri kufikisha ujumbe wa 
neon la Mungu katika Tamasha la Krismas kwani wanavifaa vipya na vya 
kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote yale 
na wafanyakazi wakutosha wenye weledi katika fani hiyo.
Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Meneja wa kitengo hicho, Alpha
 Kigalla alieleza sababu za kufanikisha vilivyo katika tamasha hilo ni 
kwa sababu ya umahiri wa  watendaji wa kirengo hicho ndio chachu 
itakayofanikisha kutekeleza ibada hiyo kwa waumini na mashabiki 
watakaojitokeza katika Tamasha hilo.
Kigalla alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini 
kujitokeza kwa wingi kushuhudia kazi za kitengo hicho kilicho katika 
kampuni ya Msama kwani wana vifaa vya kisasa zaidi.
“Msama Video Productions ina vifaa vipya na vya kisasa zaidi  na
 hata watendaji wake wako makini zaidi na utekelezaji wa kazi zao, hivyo
 wadau wa muziki nchini kujitokeza kufanikisha kazi zao,” alisema 
Kigalla.
Meneja huyo alisema wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini 
kujiandaa na kazi bora za Msama Video Productions ambazo zitafanikishwa 
kupitia waimbaji mbalimbali wa muziki huo.

No comments:
Post a Comment