
 Mgeni
 rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, 
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. 
Mary Massay akizungumza.

 Mgeni
 rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, 
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. 
Mary Massay akizindua eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili.

 Mgeni
 rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, 
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. 
Mary Massay akizungumza.

 Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.

 Maandamano
 ya washiriki wa mjadala wa kupinga ukatili, katika Maadhimisho ya Siku 
16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyoandaliwa na TGNP Mtandao jijini Dar
 es Salaam.

 Mgeni
 rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, 
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. 
Mary Massay pamoja na meza kuu wakipokea maandamano ya washiriki mjadala
 wa kupinga ukatili.

 Msanii
 Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika 
Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es 
Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.

 Msanii
 Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 
Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo 
yameandaliwa na TGNP Mtandao.
VITA dhidi ya mapambano ya vitendo
 vya ukatili wa kijinsia nchini Tanzania havina budi kuungwa mkono na 
makundi yote kutokana na umuhimu wake. Hali hii ni kutokana na kwamba 
madhara ya ukatili katika jamii yanaathiri jamii nzima bila kujali 
jinsia.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu 
Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary 
Massay katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia 
yaliyoandaliwa na TGNP na kufanyika katika viwanja vya ofisi yao, Mabibo
 jijini Dar es Salaam.
Bi. Mary Massay aliyekuwa pia 
mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa 
Kijinsia alisema kila jamii hainabudi kuanza kwa kuangalia mazingira 
inayoishi na kuona namna gani ya kupambana na vita ya nukatili wa 
kijinsia.
“…Kila mmoja analojukumu kubwa, 
vyombo vya umma/dola, taasisi za umma, watu binafsi, mitandao na 
wanaharkati wanajukumu kubwa katika kupambana na ukatili wa kijinsia, 
huwezi kuleta maendeleo kama watu wanteseka, kwa hiyo kila kundi lina 
jukumu la kupambana na ukatili wa kijinsia,” alisema Bi. Massay.
“Vita dhidi ya Ukatili wa Kijinsia
 inahitaji nguvu ya pamoja kutoka kwa wanaanchi na viongozi ngazi zote 
ili ikomeshwe. Vita dhidi ya ukatili wa kijinsia haina mwanamke wala 
mwanamume, ni lazima tupate watu wa kutosha kutoka jinsi zote 
watakaouangana kudai mabadiliko. Wanaume mlioko hapa ninyi ni wadau 
muhimu sana katika kuleta mabadiliko chanya ya kukomesha kabisa ukatili 
wa kijinsia,” alisisitiza Katibu Mtendaji huyo wa Tume ya Haki za 
Binadamu na Utawala Bora –Tanzania.
Aliwataka wazazi wasikubali 
kugeuka mawakala wa ndoa za utotoni, ambazo zimesababisha idadi kubwa ya
 wanafunzi hasa wa kike kukatishwa masomo na badala yake kuhakikisha 
wanatoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria kuwawajibisha wakosaji.
“…Msikubali kuzungumza na wabakaji
 au wanaowatia watoto mimba nje ya mahakama, mtu akishafanya kosa 
akafikishwa mbele ya sheria viachinei vyombo hivyo vifanye kazi yake, 
sheria zipo na zitatumika,” alisema.
Hata hivyo alisema zipo hatua 
zilizochukuliwa na Serikali kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwa ni 
pamoja na kurekebisha baadhi nya sheria kandamizi na kutunga sheria mpya
 zinazozingatiwa usawa wa kijinsia na haki za binadamu.
Awali akizungumza katika hafla 
hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi alizitaka 
mamlaka husika kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo la ajira nchini 
kwani limechania kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa wasichana 
hususan ule wa ajira zisizo na utu, usafirishaji haramu wa wasichana, 
biashara ya ngono, rushwa ya ngono, ndoa za utotoni na ukatili mwingine.
“…Tunasisitiza uwepo wa mabweni ya
 kutosha katika shule zote za sekondari za kata na nyigine hususan ya 
wasichana ili kupunguza umbali na mazingira hatarishi kwenda shuleni. 
TGNP Mtandao na GTI tumejitahidi kupambana na ukatili wa Kijinsia kwa 
kutoa elimu kwa Jamii katika ngazi zote, kufanya mafunzo mbali mbali kwa
 wadau mbalimbali mfano; Jeshi la polisi yakiwemo madawati ya jinsia, 
viongozi wa Dini, Viongozi wa Mila, Mahakama, viongozi mbalimbali wa 
serikali za mitaa, watendaji wa halmashauri, wahudumu wa afya, na 
wanaharakati wa ngazi ya Jamii kupitia vituo vya taarifa na maarifa 
mikoa ya Mara, Shinyanga, Morogoro, Mbeya, Dar e salaam na Pwani,” 
alisema Bi. Liundi katika hotuba yake.
Maadhimisho hayo yalioambatana na 
mijadala ya wazi kwa washiriki yalishirikisha makundi ya wanaharakati 
mbalimbali ngazi ya jamii kutoka mikoa anuai nchini pamoja na makundi ya
 wanafunzi wa kutoka jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mjadala huo 
ilikuwa “Siyumbishi, Najilinda Mnilinde” ambayo inalenga vijana kuamini 
tunaamini kuwa mapambano yanahitaji nguvu kubwa na ya pamoja.
No comments:
Post a Comment