Mwenyekiti
 wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt 
Ibrahim Msengi akifungua kikao cha tano cha bodi ya barabara Mkoa kwenye
 ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, kulia kwake ni 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe  ambaye awali alikuwa Mkuu wa 
Mkoa wa Katavi  sasa amehamishiwa mkoa wa Tanga na Nafasi yake 
kuchukuliwa na Dkt Msengi aliyemkabidhi uwenyekiti wa bodi ya 
Barabara.(Picha zote na Kibada Kibada -Katavi)  
Mkuu
 wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi Mwenye suti ya Bluu na Mkuu wa 
Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi 
wa mikutano mjini Mpanda muda mfupi baada ya kutoka kwenye Kikao  cha 
Tano cha Bodi ya  Barabara kilichofanyika leo mjini Mpanda. 
Wajumbe
 wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi wakifuatilia mjadala wa 
kikao hicho mbele ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda 
Estomhn Chang’ah mwenye suti ya kahawia na Selemani Lukanga Mkurugenzi 
wa Mji Mpanda. 
Mkurugenzi
 wa Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah akitoa taarifa ya 
utekelezaji wa miradi ya barabara kwenye kikao cha bodi ya Barabara Mkoa
 wa Katavi.
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Katavi
Mwenyekiti wa Kikao cha Bodi ya 
Barabara Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt Ibrahim 
Msengi ameshauri wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara kufanya kazi kwa 
ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha barabara za Mkoa huo zinajengwa 
kwa kiwangokinachokubaliki kuliko kukaa kinywa kusubiria hadi kikao 
kiitishwe ndiyo waseme mapungufu yaliyojitokeza.
Dkt Msengi alitoa kauli hiyo 
wakati akifungua Kikao cha tano cha Bodi ya Barabarakilichofanyika 
kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mji Mpanda 
Mkoani Katavi na kuzungumzia changamoto mablimbali zinazoikabili sekta 
ya miundo mbinu Mkoani humo hasa sekta ya Barabara.
Alisema kikao cha Bodi ni cha 
kisheria hivyo Wajumbe wake wanawajibu na jukumu la kusimamia na 
kufuatilia kazi zote zinazofanyika katika Mkoa kwa kufuata taratibu 
zinazotakiwa bila kuingilia mchakato mingine ya kisheria kama mambo ya 
zabuni na masuala ya Kifedha lakini kubwa zaidi ni ushirikiano wa karibu
 miongoni mwao taasisi nyingine kwa kuwa kila kitu kinahitaji 
ushirikiano na mawasiliano ya karibu.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema 
haitakuwa busara barabara zinajengwa chini ya kiwango na wajumbe wa bodi
 wapo waaona na kuacha kushauri hadi  kazi inakamilika ndipo wanaanza 
kuhojii wakati ungeweza kusimamia mapema na kusaidia kuondoa kasoro hizo
 kwa kutoa ushauri mapema.
Akashauri kuwa ni vyema 
ufuatiliaji uwepo tangu mwanzo ili kuhakikisha taratibu zote 
zinafuatiliwa kwa kufuata utaratibu na sheria na kuona  barabara kama 
zinajengwa kwa wakati,akaeleza kuwa hiyo ni moja ya kazi ya bodi ya 
barabara.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa 
Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo alieleza  Bodi ya Barabara Mkoa wa 
Katavi ilizinduliwa mwaka 2012 wakati linazinduliwa Mkoa ulikwa na 
mtandoa wa barabara  zinazohudumiwa  zikiwa katika hali mbaya lakini 
bodi imefanya jitihada mbalimbali na   kazi mbalimbali  zimeendelea 
kufanyika chini ya uongozi wa Bodi hii.
AIisema kazi mbalimbali 
zimefanyika na zinaendelea kufanyika akataja  barabara ya Mpanda – 
Uvinza,iko katika hali ya usanifu pia barabara ya Mpanda – Ugalla hadi 
Kaliua undyankulu Kahama, Mpanda –Inyonga, shughuli zinaendelea katika 
kuhakikisha Mkoa unafunguka.
Kwa upande wake aliyekuwa 
Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara na Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye amehamia
 Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe akimkaribisha Mwenyeiti Mpaya wa Bodi
 ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa mpya wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi ameeleza 
kuwa Mkoa wa Katavi ni moja ya Mkoa ambao uko nyuma kwa maendeleo ya 
Barabara za lami nchini hadi wakati unaanzishwa mwaka 2012 ulikuwa na 
kilometa (2)mbili za lami tofauti na maeneo mengine nchini lakini sasa 
unamtandao wa barabara za lami kilometa 34 hayo ni maendeleo kwa kipindi
 cha miaka miwili tu juhudi zimefanyika.
Amesema Mkoa una sura ya Samaki 
ya Pweza ili uende sehemu nyingine kutoka makao makuu ya mkoa lazima 
uende moja kwa moja halafu lazima urudi ulikoanzia safari  hivyo 
ameshauri wajumbe wa bodi ya Barabara na wananchi kwa ujumla 
kutoaushirikiano wa karibu kwa Mkuu wa Mkoa Mpya kama waliompatia wakati
 yeye alipokuwa mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa Bodi ya Barabara hivyo na 
mwenzake apewe ushirikianokam aliokuwa akipewa ilikuleta maendeleo 
katika Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment