TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 1, 2014

MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUMUUZIA NYUMBA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA KULEMEWA NA MADENI YA MAMILIONI YA FEDHA ALIZOKOPA

DAR ES SALAAM, Tanzania
MKE wa mlalamikaji katika kesi ya kughushi dhidi ya Mfanyabiashara Hans Macha (pichani), amedai mahakamani kwamba mumewe anadaiwa fedha nyingi na mshtakiwa, alishindwa kulipa akaamua kumuuzia nyumba.
Mke huyo Nurya Ahmad (34),ambaye ni shahidi wa upande wa utetezi, amedai hayo leo Desemba Mosi, katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, kwa kuongozwa na wakili wa utetezi, Deo Ringia.
Nurya amedai mahakamani hapo kwamba nyumba iliyokuwa ya Balenga iliyopo eneo la Kigogo, Dar es Salaam, iliuzwa kihalali kwa Macha baada ya mumewe (Balenga), kushindwa kulipa deni.
“Nafahamu kwamba mume wangu (Balenga), alikuwa andaiwa na Macha, aliniambia mwenyewe kwamba ni fedha nyingi sana, deni halikuwahi kulipwa hatimaye akaniambia kuwa ameeamua kumuuizia nyumba.
“Alikuwa akikopa kwa kuweka rehani hati za nyumba, madeni mengine yalikuwa yakilipwa, tulikuwa katika ndoa kuanzia mwaka 2001 hadi 2012, sijawahi kuona mume wangu akiwa kichaa,” alidai Nurya baada ya kuulizwa kama aliwahi kuona mumewe akiwa kichaa.
Shahidi huyo alihoji mahakamani kwamba hati za nyumba halisi zilifikaje kwa Hans Macha, kama Balenga hakuzipeleka mwenyewe kwake, aliongeza kwamba hajawahi kumsikia mumewe akilalamika  kudhulumiwa nyumba na Macha.
Mfanyabiashara Hans Macha akijitetea alidai  kwamba Ramadhani Balenga alishindwa kumlipa deni la Sh. milioni 879 akamuuzia nyumba iyo ya Kigogo.
Alidai Balengo alikuwa akimtegemea kwa kukopa fedha mara kwa mara kwa ajili ya kuingiza makontena ya vifaa vya umeme au elektroniki.
“Aliletwa na wafanyabiashara wenzangu kwa ajili ya kukopa, nilimpa masharti ya kukopa, aliweka dhamana hati ya nyumba yake ya Mabibo, Manzese, Kigogo, Mbezi Beach, mara ya mwisho Balenga nilikuwa namdai jumla ya Sh. milioni 879, wakati huo nilikuwa na hati zake za nyumba nne.
“Balenga alishindwa kulipa akidai kwamba kontena zake zilikamatwa na kufilisiwa na TRA, aliamua kuniuzia nyumba ya Kigogo, Manzese na nimuongezee Sh. milioni 20 ili tumalizane deni lote.
“Nilipofanya hivyo mbele ya wakili nilikuwa nimempa jumla ya Sh. ilioni 899, nilipomkabidhi fedha ya nyongeza Sh. milioni 20 alinikabidhi hati, siku nyingine tulisaini hati ya kuhamisha umiliki, Balenga alinikabidhi nyaraka zingine ikiwemo michoro, mikataba ya ujenzi, kibali cha ujenzi, miakataba halisi waliyoingia na kampuni ya ujenzi pamoja na risiti mbalimbali,” Macha alidai.
“Si kweli kwamba nilighushi, Balengo aliniuzia nyumba baada ya kushindwa kulipa deni, naiomba mahakama iyatupe mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yangu,”alidai Macha.
Shahidi wa tatu, Mohammed Waziri Mohammed ambaye ni mfanyakazi wa Balenga pia alidai mahakamani kwamba mlalamikaji katika kesi hiyo alikuwa akidaiwa na Macha.
Waziri alidai mara kadhaa alikuwa akienda na mlalamikaji kwa Macha kwa ajili ya kukopa fedha. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne, Desemba 2, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, KITAIFA MKOANI NJOMBE

unnamedMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, kwa pamoja wakisimama kupokea maandamano wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika leo Desemba 1, 2014 Kitaifa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe. Picha na OMR unnamed1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo, Desemba 2014. Picha na OMR unnamed5 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka katika uwanja wa Sabasaba baada ya kuhutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa huo Mkoani Njombe. Picha na OMR unnamed8Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi wakati akiondoka uwanjani hapo baada ya kuhutubia katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Njombe. Picha na OMR unnamed10Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, akijumuika na wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Kanisa la KKKT, wakati wakitoa burudani yenye ujumbe kuhusu maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi Duniani. Picha na OMR unnamed14 Baadhi ya wanadamanaji wakipita mbele ya jukwaa kuu na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu siku ya Ukimwi Duniani wakati wa sherehe hizo zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo Desemba 1, 2014. Picha na OMR unnamed15 unnamedNJO

==============================================

TMF YAFADHILI WANAHABARI TISA KWENDA ACCRA NCHINI GHANA KUPATA MAFUNZO

  on December 1, 2014 
 Wanahabari hao wanaosafiri wakimsikiliza Mkufunzi wa Masuala ya Biashara za Habari kutoka Ghana,  Nuamah Eshun.

Dotto Mwaibale
MFUKO wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), umewafadhili wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini kwenda Accra nchini Ghana kupata mafunzo. Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo katika maeneo ya utawala na uongozi, biashara, masoko na kuboresha maudhui katika vipindi vyao kama namna ya kuchochea mabadiliko ya kimfumo katika vyombo vyao.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanahabari hao wapatao 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TMF Upanga Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Ernest Sungura alisema TMF imekuwa ikiwawezesha wanahabari kupata mafunzo ya aina mbalimbali ndani nan je ya nchi.
Alisema wanahabari hao wanakwenda nchini humo ambapo watapata mafunzo kwa siku 10 kuanzia Disemba 2 hadi 13 mwaka huu.
“Waliochaguliwa kwenda kupata mafunzo hayo ni baadhi ya wakuu wa vitengo kutoka vyombo vya habari, mameneja, wamiliki wa vyombo vya habari na maofisa masoko na mauzo na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio” alisema Sungura.
Aliongeza kuwa tangu mwaka 2008 TMF imeweza kufadhili vyombo zaidi ya 120 na wanahabari zaidi ya 500 kupitia aina ya ruzuku mbalimbali. Kati ya vyombo 120 vilivyofadhiliwa na TMF, 31 vimepewa ruzuku inayolenga kuimarisha utendaji wao katika masuala ya utawala na uongozi, biashara, masoko na kuboresha maudhui katika vipindi mbalimbali.
Alisema katika safari hiyo vituo vya redio vitano vimebahatika kuchaguliwa ambavyo ni CG Fm (Tabora), Standard FM (Singida), Kahama FM (Kahama), Triple A FM (Arusha) na Jogoo FM (Songea)-(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)
================================================

Dk.BILAL KUWEKA JIWE LA MSINGI CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO

Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal (pichani) Desemba 2 anatarajiwa Kuwa mgeni
rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha
Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Kijijini Kiromo,Bagamoyo Mkoani Pwani.
 

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es
Salaam Ofisa Habari wa (UB), Happiness Katabazi alisema sherehe hizo
zitafanyika Kijijini Kilomo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na kwamba
uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha
Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao utaanza mapema Januari Mwaka 2015.

Katabazi alisema Dk. Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe
hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia
linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo ilikuwa ukikaliwa na watumwa.

” Sasa sisi UB tunaitambua hiyo historia na ndiyo maana tukaamua
kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la Bagamoyo.Na kwakuwa
kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, basi sasa kupitia UB ambayo
inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote watakuwa
huru kwasababu tutapata elimu” alisema Katabazi.

Alisema UB
ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda
,Mikocheni ,Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB
kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo
hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu.


Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla
kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo. UB ilianzishwa rasmi Mwaka
2011.

========================================================

MKUTANO KATI YA DR. SHEIN NA MABALOZI WETE KISIWANI PEMBA

 unnamed1 BAADHI ya WanaCCM  wa Wilaya ya Wete Pemba wakimkaribisha   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipofika kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa  Maskani  wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba katka ukumbi wa Jamhuri akiwa katika ziara za kuimarisha Chama .[Picha na Ikulu.] unnamed2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akitia saini kitabu cha wageni alipofika katika ukumbi wa Jamhuri Wete  kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara za Kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba leo .[Picha na Ikulu.] unnamed3Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Wete wakifuatilia kwa makini taraatibu za Mkutano huo uliofanyika leo katik na a Ukumbi wa Jamhuri  ikiwa ni katika kuimarisha Chama ,[Picha na Ikulu.] unnamed5BAADHI ya WanaCCM  wa Wilaya ya Wete Pemba wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa  Maskani  wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba katka ukumbi wa Jamhuri akiwa katika ziara za kuimarisha Chama .[Picha na Ikulu.]
unnamed6 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wete akizungumza na katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa Jamhuri Wete Pemba na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Map[induzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.] unnamed7Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea Utenzi  baada ya kusomwa  na Asha Msanif wakati wa  Mkutano wa kuimarisha Chama alioufanya leo kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya  Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.] Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.] unnamed8Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea risala ya Mabalozi  kutoka kwa Bina Khamis  wakati Mkutano wa kuimarisha Chama akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa
 on December 1, 2014 
index
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini leo (Desemba 1 mwaka huu) Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African Lyon).
Gadiel Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa Sugar).
Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.
================================================================

Shule za msingi za Rightway zaadhimishwa miaka 10 ya kuanzishwa kwake

Mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akimpa mkono Barwany Mchechu kwa kufanya vizuri katika masomo yake wakati wa mahafali ya shule ya Msingi ya Rightway, Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiwa katika picha ya pamoja na Blandina Kidda wakati wa mahafali ya shule ya Msingi ya Rightway, Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam, Kushoto kwa Mkurugenzi ni Mzazi wa Blandina Fatma Chillo na kulia kwa Blandina ni Mercy Luhanga ambaye ni Mkurugenzi washule hizo na anayemfuatia ni Meneja wa Shule hiyo Moses Kyando.
================== ===================================

Tamasha la Tigo Welcome Pack Lapagawisha Mjini Kigoma

unnamedMsanii Alex Chalamila maarufu kama MCRegan akiburudisha katika tamasha la kuhamasisha matumizi ya mtandao wa simu ya mkononi ya Tigo lililofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. unnamed1Msanii wa kundi la Origional Comedy Emanuel Mgaya (Masanja) akiburudisha kwenye tamasha la Tigo welcome pack lililofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. unnamed3Msanii wa kundi la Origional Comedy Isaya Mwakilasa (Wakuvanga) akiburudisha kwenye tamasha la Tigo welcome pack kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. unnamed4Msanii wa Bongo Flava Sunday Mjeda (Linex) akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo welcome pack lililofanyika uwanja wa lake Tanganyika mjini Kigoma. unnamed5Msanii nguli wa hiphop nchini Joseph Haule a.k.a Prof J akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo welcome pack huku akisindikizwa na wasanii wa kundi la Origional Comedy kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. unnamed6Msanii nguli wa hiphop nchini Joseph Haule a.k.a Prof J akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo welcome pack huku akisindikizwa na wasanii wa kundi la Origional Comedy kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. unnamed7 Baadhi ya wananchi wa manispaa ya kigoma ujiji wakipata huduma kuhusiana na bidhaa na huduma mbalimbali za mtandao wa simu ya mkononi ya tigo  kutoka kwenye vibanda mbalimbali vya kutoa huduma katika uwanja wa Lake Tanganyika wakati wa tamasha la Tigo welcome pack  lililofanyika mjini Kigoma.
====================================================================

Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji yafanya Mahafali ya Sita

unnamed3 Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija Kazumba (kushoto) akimkaribisha Mgeni rasmi katika maafali ya sita ya Taasisi hiyo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mgeni rasmi wa mahafali hayo.
unnamed6Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimpa tuzo mhitimu aliyeongoza katika kundi la wanawake na aliyekua na ufaulu mkukwa kuliko wahitimu wote Bi. Fatma Ngano, kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija na ushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Prof. Gabriel Roderick Kassenga.
unnamed7 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mgeni rasmi katika mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani) katika picha ya pamoja na wakufunzi na wahitimu wa Taasisi hiyo.
unnamed8 Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania Mwenge wakitumbuiza wakati wa mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) yaliyofanyika hivi karibuni.
 Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
======================================================================

BANDARI YA KASANGA KUANZA KUBORESHWA


SONY DSCKiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Watatu kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) mara walipowasili katika bandari hiyo kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo bandari hapo. SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akiwaongoza wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kujionea moja ya meli za kigeni zinazotia nanga katika bandari hiyo. Meli hiyo ni MV Rwegura kutoka nchini Burundi. SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya namna bandari yake inavyohudumia meli kutoka nchi jirani. Wanaomsikiliza ni Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi Florence Mwanri (Kushoto aliyevaa fulana nyeusi). SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) zilizopo kwenye Bandari ya Kasanga. SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akimfafanualia jambo Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakati akimkabidhi taarifa ya maendeleo ya bandari hiyo.
…………………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli, Sumbawanga
Serikali imeazimia kuanza kuiboresha bandari ya kimkakati ya Kasanga inayohudumia nchi za Burundi, Rwanda na Kongo iliyopo katika Ziwa Tanganyika, mkoani Rukwa.
Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kasanga.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania imepanga kuboresha bandari zote ili kuwa malango kuu la biashara kwa soko la ndani na kwa nchi jirani ili kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena kwa ufanisi.
“Tumedhamiria kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo Bandari ya Kasanga ili kuweza kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma katika eneo hili,” alisema.
Bibi Mwanri aliongeza kuwa serikali pia imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Kasanga na Kigoma na kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa bandari mpya za Mwambani (Tanga), Mbegani (Bagamoyo) na Bandari Kavu ya Kisarawe.
Akizungumza na ugeni huo, Msimamizi Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa alisema kuwa Bandari hiyo ina fursa nyingi katika kuhudumia shehena na abiria wanaopitia bandarini hapo.
“Bandari yetu ina fursa kubwa za kibiashara kwani tuna wateja wengi kutoka ndani na nje ya nchi wanaotumia bandari yetu kupitishia bidhaa zao, pamoja na abiria wanaosafiri kwenda nje na ndani ya Tanzania,” alisema.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha Serikali imedhamiria kuboresha mazingira yatakayowezesha sekta binafsi kuwekeza katika kujenga miuondombinu na kuboresha usafirishaji wa mizigo katika bandari zote nchini.
Pia, Mpango huo unaweka bayana kuendeleza na ukarabati na ununuzi wa vyombo vya usafiri na usafirishaji katika maziwa.
=================================================================

PONGEZI KWA MSANII NASSIB ABDUL AKA DIAMOND KWA KUSHINDA TUZO TATU ZA CHOAMVA14

1976886_842456352442847_3553307454253637477_n
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo tatu kwa mkupuo za CHOAMVA zinazoendeshwa na kituo maarufu cha luninga cha Channel 0 chenye makao makuu yake Afrika Kusini.
Tuzo alizoshinda Diamond ni pamoja na Most Gifted East African Artist, Most Gifted Afro Pop video na ile ya Most Gifted New Comer.
Kushinda kwa Diamond katika tuzo hizo kubwa barani Afrika na kuwashinda wasanii wengine wenye ‘majina makubwa’ ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na
Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kujitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Aidha, Baraza linaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wadau wa muziki na Sanaa kwa ujumla hususan wakuzaji Sanaa (mapromota) kuendelea kujenga mazingira rafiki kwa wasanii wetu kufanya kazi kwa ubora na weledi lakini pia kwa upendo na furaha ili kujenga daraja zuri kwa wasanii wengi zaidi kung’ara kwenye ngazi za kimataifa.
Ni imani ya Baraza kwamba, ushindi huu wa kihistoria wa Diamond utakuwa chachu kwa wadau wote wa Sanaa nchini hususan wasanii katika kujituma na kuhakikisha hawaridhiki na mafanikio waliyonayo.
Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii na wadau wote wa Sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji sekta sambamba na kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
====================================================================

Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar

SONY DSCMkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto mbele), wakiwaongoza wafanyakazi wa Airtel Tanzania na wanafunzi kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel , Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. SONY DSCMkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani, funguo za kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto), na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Mwemba Mwilima. SONY DSCMkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akifungulia maji ya bomba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa  kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa nne kushoto).
………………………………………………………………………….
 Yaendesha matembezi yahisani kuendelea kuboresha mazingira ya shule
  • Zaidi ya shilingi milioni 10 kukusanywa
Dar es salaam Novemba 30, 2014 Kampuni ya Airtel leo imeendesha matembezi ya hisani ili kuchangisha  pesa kwajili ya kuendelea kuboresha shule ya msingi kumbukumbu iliyopo jijini Dar es salaam 
Matembezi yenye lengo la kupata pesa ili kufanya ukarabati wa darasa la watoto na kununua viti na meza za kukalia yameetimishwa kwa uzinduzi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na wafanyakazi wake ili kukabiliana na tatizo la maji shule hapo
Akiongea wakati wa kuzindua kisima hicho mgeni rasmi , Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya jamii  jinsia na watoto Mh. Sophia Simba alisema”  naunga mkono juhudi zilizofanywa na Airtel katika kuendelea kuboresha mazingara ya utoaji elimu shuleni hapa. Nimefurai kuona kuwa Airtel haikuridhika na ujenzi wa kisima hii tu bali wameamua kuchua hatua nyingine ya kushirikisha wadau mbalimbali katika kutatua changamoto walizoziona shuleni hapa.
Leo tumetembe kwa pamoja ili kuweza kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 10 zikazowesha kazi ya kuendelea kuboresha mazingara ya shule hii kuendelea. 
Serikali inaunga mkono dhamira hii na jitihada hizi zinazoenda sambamba na kauli mbili yetu ya Matokeo makubwa sasa  na kuhakikisha tunaboresha maeneo muhimu hususani elimu kwani vijana hao ndio nguvukazi na taifa la kesho. Natoa wito kwa mashirika mengine watu binafsi na taasisi mbalimbali kujitokeza na kuchangia katika shughuli za jamii ili kukubiliana na changamoto tulizo nazo sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” nawashukuru wafanyakazi wa Airtel na kila moja aliyeshiriki hapa kwa kujitoa katika kusaidia jamii, sisi Airtel tumejipanga kutimiza dhamira yetu ya kuchangia katika kuhakiksha tunachangia katika sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa vitabu na kuboresha mazingira ya shule. Kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifika shule nyingi kwa kuwapatia nyenzo muhimu katika elimu na leo tumewafikia shule ya msingi kumbukumbu tukiwa na lengo na kuendelea kuboresha sekta ya elimu.
Mpango huu wa Airtel Tunakujali ni endelevu bado tutakuwa  shughuli nyingi zaidi na shule nyingi zikipokea misaada hivyo tunawaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana nasi.
Kwa upande wake mfanyakazi wa Airtel Bi Veneranda Boniface Alisema amejisikia furaha kutumia jumamosi yake kutembea kwaajili yakusaidia jamii, hii ni sehemu pia ya mazoezi lakini zaidi ni njia pekee ya kuniwezesha mimi kwa nafasi yangu katika jamii kushiriki kuchangia.
Matembezi hayo ya hisani yalianzia katika makao makuu ya Airtel yaliyoko Moroco Dar esaalam na kwenda njia ya Alihasan Mwinyi, kupitia Kaunda, Bongoyo , haileselaile , Ali hassani Mwinyi na kuishia katika shule ya msingi Kumbukumbu.
==================================================================

AJALI ZA BARABARANI ZAONGEZEKA TABORA ZAUWA IDADI KUBWA YA WATU!!!

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akipata maelezo kutoka kwa Dr.Anna Kichambati wa Redcross Tabora wakati wa sherehe za wiki ya usalama barabarani mkoani Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akisalimiana na Afisa mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Tabora Bw.Joseph Michael wakati wa wiki ya usalama barabarani mkoa wa Tabora
Mmoja kati ya maafisa wa polisi kikosi cha usalama barabarani Tabora mjini akimuonesha mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila kifaa maalumu kinachotumika kupima kiwango cha ulevi kwa madereva wazembe.
Kikosi cha zimamoto mkoa wa Tabora kikionesha vifaa vinavyotumika wakati wa uokoaji ajali zinapojitokeza.
Sherehe za wiki ya usalama barabarani mkoa wa Tabora zilianza kwa maandamano yaliyopita mitaa mbalimbali hadi viwanja vya mazoezi ya Jeshi la Polisi Tabora ambapo wananchi walishiriki maandamano hayo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kikosi cha usalama barabarani SSP Peter Mnyandwa akitoa taarifa ya ongezeko la  ajali za barabarani mkoani Tabora ambapo zaidi ya watu 150 wamefariki dunia katika ajali 399 huku watu 520 wamejeruhiwa katika ajali 185.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akihutubia katika sherehe hizo za wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambapo mbali ya kusikitishwa na taarifa ya ajali hizo lakini alisema kuwa asilimia 75 ya ajali hizo zinatokana na makosa ya kibinadamu na hivyo kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua ya kudhibiti kupunguza ajali hizo ikiwa ni pamoja na kutotoa leseni kwa madereva ambao hawajapata mafunzo ya udereva darasani.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti mstaafu wa Kamati ya Usalama barabarani mkoa wa Tabora Bw.Moshi Abrahamu maarufu Nkonkota.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akikabidhi cheti cha pongezi kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya NBS kwa usafirishaji salama bila kusababisha ajali kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.
 ==============================================================

UNESCO WAANZISHA PROGRAM YA UTAMADUNI KUKABILI UKIMWI

DSC_0202Afisa Ardhi na Mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala (Kahama), Zablon Donge, akifungua rasmi warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo, iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias.
Na Mwandishi Wetu, Kahama
MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ametaka jamii kujumuisha suala la utamaduni katika kupambana na maambukizi mapya ya Ukimwi.
Alisema hayo kwenye warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI inayofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Alisema katika ufunguzi huo kwamba kwa miaka mingi pamoja na kuwepo kwa elimu ya UKIMWI, kumekosekana mabadiliko yanayotakiwa kukabili maambukizi mapya.
Alisema UNESCO iliangalia tatizo hili na kubaini kwamba kutobadilika kwa hali kumetokana na kutounganishwa kwa kipengele cha mila ambacho ndicho kinachofanya kuwepo na mazingira rafiki ya kupashana habari.
DSC_0151Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na washiriki wakati wa uzinduzi wa program ya utamaduni kukabili UKIMWI itakayoendeshwa na shirika lake.
Warsha hiyo ya Siku tatu imelenga katika kuhamasisha jamii, Shule, Asasi, Taasii za Dini na Serikali katika utoaji wa Elimu sahihi ya huduma rafiki za Afya ya Uzazi, VVU/UKIMWI, ujinsia na maadili ya Afya kwa vijana balehe na vijana.
Amesema mpaka sasa utoaji wa elimu ya afya, ueleweshaji wa ugonjwa haujafanya mabadilikoya kutosha kutokana na ukweli kuwa katika utekelezaji wa kampeni masuala ya utamaduni na uwasilishaji wa taarifa haukuwa umezingatiwa.
Alisema wakati Kahama (Msalala) kwa sasa kiwango cha maambukizi ni asilimia 5.9, Juhudi zinatakiwa kufanywa katika kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa inahusishwa na masuala ya kitamaduni ili kubadilisha maisha ya wakazi.
Alisema katika mapambano ya maambukizi mapya mila na utamaduni zinaweza kabisa kusaidia kukabiliana na maambukizi ya UKIMWI.
DSC_0348Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akielezea madhumuni ya warsha hiyo ya siku tatu iliyojumuisha makundi mbalimbali ikiwemo Waganga wa jadi, wakunga wa jadi, viongozi wa dini, viongozi wa vijiji na kata, walimu, wataalamu wa afya na elimu na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
Alisema program inayoangaliwa sasa ni ile iliyoleta mafanikio katika nchi kadhaa za Afrika ikiwamo Msumbiji na hivyo wanaona waijaribu Tanzania katika wilaya sita ikiwemo Kahama na hasa halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Alisema pamoja na watu wengi kutibiwa na waganga wa kienyeji ni vyema watengeneza sera na watu wengine kutambua umuhimu wao ili kwa kupitia mila waweze kuwafunua watu akili na kujikinga na maambukizi ya UKIMWI.
Alisema anaamini kuwa mila na tamaduni zikitumika vyema na hata matibabu zitasaidia kuokoa maisha ya wengi na pia kuzuia maambukizi mapya.
Alisema maambukizi mapya ni tatizo kwa sasa hasa ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wanajua uwapo wa UKIMWI lakini ufahamu ni mdogo kwa kuwa katika kufundisha watu hawakupewa elimu ya kutosha inayoambatana na kuangalia mila na desturi njema za afya zilizopo.
DSC_0366Afisa afya mkuu kitengo cha elimu ya afya kwa umma-programu ya afya mashuleni kutoka Wizara ya afya na ustawi wa jamii, Avit Maro akielezea jambo kwa washiriki kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi wakati wa warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Alisema ni vyema wananchi wakatumia mali asili waliyonayo kufundishana juu ya kukabiliana na maambukizi mapya ya UKIMWI.
Alisema UNESCO imeamua kuanzisha programu maalumu ya kutumia mila na desturi kukabili UKIMWI kama njia nyingine ya kuoanisha nguvu katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala (Kahama), Zablon Donge alishukuru UNESCO kwa kuanzisha program ya kujifunza namna ya kukabiliana na maambukizi mapya ya UKIMWI.
Alisema ukiwa na halmashauri ya wagonjwa huwezi kuwa na halmashauri kwa kuwa shughuli za kiuchumi na kijamii kushindikana kutekelezwa, na kusema kuja kwa UNESCO ni msaada mkubwa.
Warsha hiyo imejumisha makundi mbalimbali ikiwemo Waganga wa jadi, wakunga wa jadi, viongozi wa dini, viongozi wa vijiji na kata, walimu, wataalamu wa afya na elimu na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
DSC_0384Mkurugenzi msaidizi masuala mtambuka kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, Dkt. Laetitia Sayi akifafanua jambo jinsi wizara yake inavyoshirikisha jamii katika utoaji wa elimu mashuleni hususani afya ya uzazi, VVU/UKIMWI huku ikishirikiana na wadau wao wa karibu UNESCO.
DSC_0269Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akiendesha warsha hiyo kwa njia ya majadiliano na washiriki juu ya dhana na maana ya balehe, vijana balehe na vijana sambamba na maana ya mimba na ndoa za utotoni.
DSC_0368Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki hao wakifuatilia majadiliano kwenye warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
DSC_0063
DSC_0257Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wakichangia maoni wakati majadiliano ya kutafuta suluhu ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI, mimba na ndoa za utotoni kwenye jamii zao.
DSC_0264
DSC_0096Sehemu ya washiriki warsha hiyo kwenye vikundi kazi wakianisha na kubainisha matatizo yanayowakabili vijana balehe na vijana katika jamii zao huku wakiongozwa na Mkurugenzi msaidizi masuala mtambuka kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, Dkt Laetitia Sayi (kushoto).
DSC_0091Mshiriki akiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano.
DSC_0061Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua baadhi ya changamoto zilizoanishwa kwenye vikundi kazi na washiriki wakati wa warsha hiyo ya siku tatu.

SUNDERLAND 0 CHELSEA 0 AND TANZANIA 1

unnamed unnamed2
By Ayoub Mzee-London
Tanzania Tourist Board was in the UK to launch a series of events related to the promotion of Tourism In Tanzania at Sunderland FC .The day also saw the launch of ‘a holiday of a lifetime’ campaign to visit Tanzania .
The day saw Sunderland players wearing special t-shirts ahead of the home draw with Chelsea as part of the club’s partnership with Tanzanian Tourist Board.
The Black Cats took to the field in the pre-game warm up sporting shirts emblazoned with the ‘Visit Tanzania’ logo as part of the partnership.
SAFC has already developed close links with Tanzania, through providing technical and practical support to the development of the football academy project, the first of its kind in the country.
The project will see thousands of youngsters benefit from a joined up approach combining football, education and community engagement, harnessing the knowledge and expertise of Sunderland AFC and its own successful Academy.
Present at the event was the Tanzania High Commissioner HE Peter Kallaghe ,the Chairperson of the board of Governors of TTB ,TTB’s Marketing Manager Devota Mdachi and other members of TTB team
For more details visit www.safc.com/tanzaniaholiday
========================================================================

MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI

unnamed Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi  wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR
unnamed2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR
unnamed3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR
unnamed4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo.
unnamed5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR
………………………………………………………………………………
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
 
Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
 
Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
 
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
 
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
 
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu – Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
 
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
 
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
 =======================================================================

TRA ARUSHA YAVUKA MALENGO

TRA1(20)Na Gladness Mushi,Arusha
MAMLAKA ya mapato Tanzania( TRA) mkoani arusha imevuka kiwango cha
makusanyo ya kodi kutoka bilioni 205.1 kwa mwaka 2012 /2013 hadi
kufikia bilioni 244.2 kwa mwaka 2013 /2014 huku wakitarajia kukusanya
bilioni 293.3 kwa mwaka 2014 /2015.
Hayo yalisemwa jana na meneja wa mamlaka ya TRA mkoani hapa Evarest
Kileva alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mlipa kodi
yaliyofanyika katika viwanja vya makumbusho vilivyopo jijini hapa.
Kileva alisema kuwa mafanikio hayo yalitokana na jitihada za mamlaka
hiyo kuwahimiza wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi katika
kukuza pato la taifa .
Alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikitambua umuhimu wa walipa kodi na
hivyo kuamua kuwazawadia wale wote waliofanya vizur katika kutimiza
wajibu wao kulipa kodi kwa kupeana mkono ili kuhamasisha na wengine
waweze kujua umuhimu wa ulipaji kodi.
Aliongeza kuwa mamlaka hiyo kwa sasa Imejipanga kuongeza jitihada kwa
kufanya kazi kwa bidii ili kuvuka malengo waliyokusudiwa katika
kuhakikisha wafanyabiashara wadogo na wakati wanalipa kodi kwa wakati
ili kuwezesha pato la taifa lizidi kuongezeka
Akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa,mkuu wa
wilaya ya monduli Jowika Kasunga alitaka mamalaka kuhakikisha
inathibiti wafanyabiashara ambao hawalipi kodi kwa wakati kwani swala
hilo ni la kisheria .
Kasunga alidai kuwa ngezeko hili ni kubwa sana tofauti na ongezeko la
mwaka lililopita hivyo kuitaka mamlaka hiyo kuzidi kuongeza jitihada
za kutoa elimu zaidi kwa walipa kodi pamoja na wafanyabaishara ili
kuweza kuvuka hata malengo waliyojiweka ya ukusanyaji mapato kwa mwaka
huu.

NHIF WAZINDUA KAMPENI YA MFUKO WA AFYA YA JAMII VIJIJI VYA NZEGA

Mkuu
wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akipokea msaada wa shuka kwa ajili ya
wagonjwa wa Zahanati ya kijiji cha Ubinga zilizotolewa na Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ambapo Afisa Matekelezo wa mfuko
huo Sunday Matoi alikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Nzega kabla
ya kufanya ufunguzi wa majengo mapya ya zahanati ya Ubinga..

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMPA MWAKYEMBE MWEZI MMOJA KUTOA MAJIBU KWA NINI MAZAO YA KOROSHO NA UFUTA HAYASAFIRISHWI NJE KUPITIA BANDARI YA MTWARA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Mtwara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye  viwanja vya Mashujaa mjini humo akihitimisha ziara yake ya siku 16 aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi wenyewe na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo Katibu mkuu huyo aliongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Katika kutano huo Kinana amempa wiki mbili Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe kutoa maelezo kwanini bidhaa mbalimbali hazisafirishwi kwenda nje kupitia bandari ya Mtwara, Lakini pia Kinana amewaagiza Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ni kwanini wawekezaji wenye kampuni zinazofanya shughuli zao mtwara wanalipia kodi zao jijini Dar es salaam badala ya kulipia mkoani Mtwara ambako wanafanya shughuli zao, Pia waziri wa Ofisi ya Mkamu wa Rais Mazingira amepewa mwezi mmoja kuhakikisha dampo la taka za sumu zinazotupwa na wachimbaji wa gesi na viwanda kuacha mara moja kwa sababu zinahatarisha maisha ya wakazi wa Mtwara, Mwisho akaagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa kibali cha kugawa viwanja katika manispaa ya Mtwara kwani viwanja vimeshapimwa, Fedha za kulipa fidia zipo ila kibali kutoka ofisi ya Waziri mkuu ndiyo kimkwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
 Wananchi wakinyoosha mikono yao juu kufurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiwahutubia.
 Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji akiwahutubia wapiga kura wake ambao walifurahia sana hotuba yake kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
 Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakati wa mkutano huo.
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
 Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape nnauye wakiingia katika uwanja wa mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangali vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia Nape Nnauye na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakiwasili katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara leo.
===============================================================

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ATOA HESHIMA KWA SHUJAA ALIYETUNGUA NDEGE MBILI ZA KIRENO WAKATI WA VITA YA UKOMBOZI WA NCHI YA MSUMBIJI

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima zake katika mnara wa Shujaa wa vita vya ukombozi wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji mwanajeshi wa Tanzania Marehemu Ahmad Mzee aliyeuwawa na wanajeshi wakoloni wa  Kireno waliokuwa wakitawala nchi ya Msumbiji mwaka 1972 wakati akilinda mipaka ya Tanzania na kifaru kandokando ya mto Ruvuma katika kata ya Kitaya Mtwara vijijini, Mwanajeshi huyo alifanikiwa kuangusha ndege mbili za mreno aina ya Jet Fighters zikitokea Msumbiji katika kijiji cha Kitaya, ambapo na yeye alijeruhiwa baada ya kupigwa na wareno hao na kukimbizwa katika hospitali ya Mtwara ambapo baadaye alifariki dunia, Katibu Mkuu Kinana yuko katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara akikagua ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali, Huku akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma ujumbe uliopo katika mnara huo ukimuelezea shujaa Ahmad Mzee. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara. 4Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kitaya. 5Baadhi ya wageni  kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakiwa katika mkutano wa hadhara wananchi wa Kitaya waliwaalika majirani zao wa Msumbiji kuhudhuria katika mkutano huo. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kata ya Kitaya Mtwara vijijini. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza wakati  akiwahutubia wananchi katika kata ya Kitaya Mtwara vijijini. 8Mkuu wa wilaya ya Wilman Ndile akiwahutubia wananchi. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaguamajengo ya kituo cha afya cha Nanguruwe Mtwara vijijini. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi katika kituo cha afya cha Nanguruwe Mtwara vijijini. 11Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdlrahman Kinana hayupo pichani katika kijiji cha Naguruwe 13Baadhi ya mabango yakionyesha Mabango yanayoonyesha ujumbe wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Huu ndiyo mnara wa Shujaa Ahmad Mzee katika kijiji cha Kitaya. Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kitaya Mtwara vijijini leo.
=====================================================================

SHULE YA SOUTHERN HIHGHLANDS MAFINDA YAOMBA WADAU KUCHANGIA SEKONDARI MPYA YA MUFINDI HIGHLANDS SCHOOLS

WAZAZI   na  wadau  wa  shule ya  kimataifa ya Southern Highlands Mafinga  mkoani Iringa  wanataraji kukutana  kesho  kwa ajili ya  kutathimini ufaulu  mzuri wa wanafunzi shuleni hapo na kuichangia  shule   hiyo ili  kuendeleza  ujenzi wa  shule mpya ya  sekondari  inayofahamika kama  Mufindi Highlands Schools ambayo inataraji  kuanza rasmi mwakani 2015
Hatua  ya  shule   hiyo  kukutanisha  wadau na wazazi imekuwa  ikifanyika  kila mwaka ila kwa  mwaka   huu wanataraji kuitumia   siku hiyo ya  wazazi wa  wanafunzi wanaosoma na  waliosoma  shuleni hapo kufanya harambee  kama  njia ya kuunga mkono   jitihada za  elimu  zinazofanywa na uongozi  wa  shule  hiyo.
Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima Mkuu  wa  shule  hiyo Joson Nyabuto alisema  kuwa  zoezi hilo  litafanyika mapema  kesho na hivyo kuwaomba  wadau kujitokeza  kushiriki harambee  hiyo yenye lengo la kuinua kiwango cha  elimu ya  sekondari wilaya ya Mufindi.
Kwani  alisema kuwa  kuanzishwa kwa  shule  hiyo mpya ya  sekondari  katika  wilaya ya  Mufindi ni mafanikio makubwa katika  sekta ya  elimu na ni jambo la kujivunia kwa  kila mdau wa  elimu ndani ya  wilaya hiyo ni nje ya  wilaya ya Mufindi.
Kwani  alisema  kwa mwaka huu katika  wilaya ya Mufindi wazazi  wawe na  imani ya  wanafunzi  wote  watakaofanya  vizuri mtihani wa darasa la saba ambao watateuliwa  kujiunga na sekondari  nafasi  zipo pia katika  shule  ya sekondari ya Southern  Mafinga ambayo ni ujio mpya wa shule za sekondari katika  wilaya ya Mufindi huku moto  wake  ukiwa ni kufaulisha kwa  kiwango  cha juu.
Hata   hivyo  mkuu  huyo alisema kuwa  shule  hiyo kwa mwaka  huu   2014 ilikuwa na  wanafunzi 48 na wote  walifaulu kujiuga na  sekondari na kuifanya  shule  hiyo katika matokeo ya mtihani  huo  kitaifa kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kati ya  shule 167  kimkoa nafasi ya nane kati ya shule 458  na kitaifa kuwa  shule ya 353 kati ya  shule zaidi ya 15,867 hivyo kwa matokeo  hayo shule  hiyo imeweza kupanda kwa wastani wa pointi tano  zaidi ya mwaka jana .
  Alisema kwa mwaka jana shule  hiyo ilifaulisha  pia  wanafunzi wote  47  na kushika nafasi ya pili  kiwilaya  nafasi ya  9 kimkoa na kitaifa  kuwa shule ya  288.
 
Pia alisema ni muda umefika wa  ndoto ya  shule  hiyo kuanza  kufanya  kazi  kuendesha  shule  yake ya  sekondari kuanzia mwakani.
Akielezea  mikakati ya mbeleni katika kuwawezesha  watoto  wanaosoma  katika  shule hiyo mkurugenzi mtendaji Bi Mary Mungai  alisema  kuwa  tayari ujio wa  shule ya  sekondari  inayofahamika kwa jina la Mufindi Highalnds Schools ambayo  kuanzia  mwakani inaanza  kupokea  wanafunzi wa kidato  cha kwanza .
Alisema  kuwa ombi la  kuanzisha  shule ya  sekondari  lilitolewa na  wazazi wa  wanafunzi  wanaosoma katika  shule  hiyo ili kuepuka watoto  wao kwenda kupata  elimu ya  sekondari  mbali na mikono ya shule  hiyo ya  Southern Highlands Mafinga na  kuwa  tofauti ya  shule  hiyo  ya  sekondari na shule  nyingine ni unafuu wa ada na ubora  wa elimu itakayotolewa lengo  likiwa ni  kuifanya  wilaya ya Mufindi kuendelea  kuwa  kisima cha elimu  bora nchini.
====================================================================

DR. SHEIN AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA NA MAKATIBU ZANZIBAR LEO

unnamed6Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Bw.Khamis Jabir Makame  kuwa  Mkuu  wa Wilaya ya Kusini Unguja  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ikulu.]unnamed1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Bw.Haji Makungu Mgongo  kuwa  Mkuu  wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.]unnamed2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Bw.Hassan Khatib Hassan kuwa  Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed3 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi Madina  Mjaka Mwinyi kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Said Seif Mzee kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Juma Yakout Juma kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Khadija Bakari Juma kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed10Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati)akiwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa wakifuatilia kwa makini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwwapisha Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali na Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo, [Picha na Ikulu.] unnamed9Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali wakifuatilia kwa makini walipokuwa wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, [Picha na Ikulu.] unnamed8 Mwanasheria Mkuu wa Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Hassan Said(kulia) akiwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria  katika Viapo mbali mbali vya Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu wa Serikali waliapishwa leo na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] unnamed7Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali wakifuatilia kwa makini walipokuwa wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
=================================================================

Lamudi Tanzania kutangaza huduma za madalali bure

Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Lamudi Tanzania, imetambulisha huduma yake ya kuwawezesha madalali mbalimbali wanaofanya kazi ya kuwatafutia nyumba, viwanja na magari wateja wao ili kuweza kutangaza huduma wanazotoa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma amesema kwa sasa madalali wanaweza kutangaza nyumba, viwanja na magari yaliyoko sokoni kupitia mtandao wa kampuni hiyo bila malipo yoyote.
Akifafanua zaidi Lemma alisema dalali anayependa kupata huduma hiyo anatakiwa kufika katika ofisi za Lamudi Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam (Garden Road) na kujaza fomu ambayo itaelezea huduma yake na kuanza kuitangaza kwenye tovuti www.lamudi.co.tz bila malipo yoyote.
“…Kimsingi huduma hii inawasaidia sana madalali kutangaza kazi walizonazo, bei zao na hata eneo ilipo. Mfano kama ni nyumba au kiwanja baada ya dalali kutoa taarifa za kutosha sisi tunamtangazia bure kazi hiyo kupitia tovuti yetu (www.lamudi.co.tz),” alisema Lemma.
Alisema mbali ya kuwasaidia madalali kutangaza bidhaa zao wameanza kutoa pia mafunzo ya kuwajengea uwezo madalali kuweza kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi ili kujenga heshima ya kazi zao.
“Wakati mwingine tumekuwa tukifanya kazi ya kuchukua baadhi ya madalali na kuwajengea uwezo, kuwapa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi na masuala mengine ya msingi katika shughuli zao,” alifafanua Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja.
Pamoja na hao alisema kwa sasa kampuni ya Lamudi Tanzania imezinduwa huduma mpya ya kumwezesha mteja kupata taarifa za uuzaji au ukodishaji nyumba ama viwanja kupitia simu za mkononi hivyo kumrahisishia kupata taarifa kwa wakati.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
=================================================================

MAXCOM AFRIKA YATIMIZA MIAKA MITANO, YABADILI MUONEKANO WA HUDUMA YAO YA MAX MALIPO

 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya  MaxCom Africa, inayotoa huduma za Max Malipo,  Juma Rajabu  na Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula wakikata utepe kuzindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo, katika hafla iliyokutanisha uongozi wa kampuni hiyo ya Jukwaa la Wahariri, leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akizindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo itakavyokuwa sasa kwenye ofisi za mawaakala wake.
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula, kuashiria kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa la Wahariri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max
Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa
Mwakilishi wa Manispaa ya Ilala Mashauri Saidii, kuashiria kampuni
hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika
shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo
kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa
la Wahariri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya MaxCom Africa, Juma Rajabu akishikana mkono na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevile Meena baada ya kutangaza kulichangia Jukwaa hilo sh. milioni 5
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya  MaxCom Africa, Juma Rajabu (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mwishoni mwa mazungumzo yaliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kushoto ni Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevile Meena
 Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, Juma Rajabu akizungumza na wahariri Serena hotel 
 Ofisa Mkuu wa Operesheni, wa Maxcom Africa, Ahmed Rusasi akieleza huduma za Max Malipo zitolewazo na kampuni hiyo, wakati wa kikao hicho na wadau katika hoteli ya Serena jijini DSar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MaxCom Afrika akiwa ameketi meza kuu na wadau
 Baadhi ya viongozi wa Maxcom Afrika katika hafla hiyo
 Wadau kutoka Jukwaa la Wahariri
 Wadau kutoka Jukwaa la Wahariri
 Wadau kutoika jukwaa la wahariri
Baadhi ya waalikwa kutoka Jukwaa la wahariri wakipata chakula cha mchana ambacho kilitoplewa kwa wote katika hotelo ya Serena jijini Dar es Salaam, baada ya uongozi wa MaxCom Afrika kumaliza mazungumzo yao na wadau katika kuadhimisha miaka mitano ya kampuni hiyo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
===================================================

CLARIFICATION ON 2014 CECAFA CHALLENGE CUP EDITION

index
The New Vision [Uganda] of this Friday November 28, 2014 has run a news story on Page 49 titled ‘CECAFA SHOW OFF’ under which the author indicated that this year’s CECAFA edition won’t take place.
As much as the author doesn’t clearly indicate the source of his information for the alleged call-off of the regional event, he somewhere claims to have spoken to me yesterday [Thursday] which never happened.
I therefore wish to clarify as follows:
1. It’s true, this year’s CECAFA challenge Cup had been scheduled for Ethiopia but the intended Member Association later showed inability to host the event.
2. The CECAFA Executive Committee headed by Eng. Leodgar Tenga and the Secretary General Mr. Nicholas Musonye are still working out the possible measures to ensure that a late championship is at least organized.
3. CECAFA will later officially communicate its position on this matter.
4. CECAFA therefore wishes to ask all journalists and Media Houses to consult the relevant authorities before running personal opinions attributed to CECAFA officials.
Anticipating your continued cooperation as we jointly work together for the development of our game.
Yours
ROGERS MULINDWA
CECAFA MEDIA MANAGER
+256 772 751 829/ +256 701 520 115
=============================================================

WIZARA YA AFYA YAKABIDHIWA MAGARI MAPYA

unnamed1Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donald Mmbando (kushoto)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari   leo  baada ya kupokea msaada  wa magari manne na vifaa vya afya  kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya  la Dunia(WHO),Dk. Rufaro Chotaro(kulia). unnamed3Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donald Mmbando (kushoto)akipokea mojaya funguo kati  ya magari manne kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya  la Dunia(WHO),Dk. Rufaro Chotaro(kulia)
unnamedBaadhi  ya   wa magari hayo .

Serikali imesema inatambua VICOBA kama mkombozi wa wanyonge nchini.

=========================================

index
Na Eleuteri Mangi- Dodoma
Serikali imesema kuwa VICOBA ni taasisi binafsi inayomilikiwa na wananchi wenyewe vikiwa ni miongoni mwa tasisi ndogo za kifedha ambazo ni za kibinafsi na huanzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa ama kijijini, kitongojini na hata kwenye kata.
Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rungwe Magharibi Prof. David Mwakyusa (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali inatambua VICOBA  kama mkombozi wa wanyonge.
Mwigulu amefafanua kuwa taasisi hizo zimo kwenye sekta ya fedha isiyorasmi na zinatoa huduma za kifedha mijini na vijijini.
 “Uwepo wa taasisi hizi, umewezesha kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi waliombali na huduma za sekta rasmi ya fedha na hivyo kuwa mkombozi wa wanyonge” alisema mwigulu.
Aidha, kwa kutambua suala hilo, ili kusaidia na kuimarisha taasisi hizo, Mwigulu amesema kuwa Serikali baada ya kupata ushauri kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa masuala ya uchumi na tafiti za kijamii, inafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Taasisi ndogo za huduma ya fedha ya mwaka 2000 ili kuihuisha iweze kukabili na kuzingatia mabadiliko na maendeleo yanayojitokeza katika sekta hiyo.
Vilevile Mwigulu amesema kuwa Serikali inakamilisha uhuishaji wa sera ya taasisi ndogo ndogo za kifedha ambapo hatua inayofuata ni kuandaa mapendekezo ya muswada ambayo yatapelekwa Baraza la Mawaziri mara baada ya kupata idhini na maelekezo ya Baraza hilo na muswada huo utafikishwa bungeni.
Taasisi ya VICOBA ilianzishwa nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo imekuwa na manufaa kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini hususan wanawake waishio vijijini wamefanikiwa kuboresha kipato chao na maisha yao kwa ujumla kwa kujiunga na taasisi hiyo.
=================================================================

WAWEKEZAJI WA MAKAMPUNI YA UBELGIJI WAFANYA ZIARA ZANZIBAR.

unnamed Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji Dkt. Diodorus B. Kamala akielezea lengo la ujio wa wawekezaji kutoka Ubelgiji kuja kuwekeza nchini Tanzania alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ujio wa wawekezaji wa nchi hiyo Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar unnamed1Waziri wa Miundombinu na Mawasilino Juma Duni Haji akiwa na watendaji wake wakuu wakimsikiliza Meneja mauzo  wa Kampuni ya ujenzi ya Anglo Belgian Corporation ya Ubelgiji walipofanya mazungumzo Ofisini kwake Kisauni.
 Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akizungumza na ujumbe wa Wafanyabiashara  wa Makamupuni ya uwekezaji kutoka Ubelgiji walipomtembelea Ofisini kwake  Vuga Mjini Zanzibar. unnamed6 
Picha ya pamoja ya wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na viongozi  wa Mamlaka ya Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar  (ZIPA).(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
=======================================================================

Msanii wa Komedy wa Nigeria awasifu wasanii wa Tanzania

index
Na  Mwandishi Wetu
MSANII wa vichekesho (komedy) kutoka Nigeria,Okopcha Bright Onyekere maarufu kama Basket Mouth amewasifu wasanii wa Tanzania kwa juhudi wanazofanya kuelimisha jamii kutumia vipaji vyao.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kuwasili kutoka Nigeria kwa ajili ya onesho maalum kushirikiana na wasanii wa Tanzania juzi Dar es Salaam alisema kutoka aanze sanaa ya vichekesho miaka 16 iliyopita amekuwa akipata sifa za wasanii wa Tanzania wakiwika katika fani za muziki, sanaa za filamu, michezo ya kuigiza na vichekesho.
Onyekere aliyetamba nchini Nigeria na Bara la Afrika katika fani hiyo amekuja kufanya onesho moja lililopangwa kufanyika jana hoteli ya Golden Tulip, aliongeza kuwa sanaa ni utajiri mkubwa kama vipaji walivyopewa vitatumika ipasavyo na kutawala jukwaa .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku alisema lengo la kumleta msanii huyo wa komedy ni kuimarisha sanaa ya vichekesho kwa wasanii chipukizi wa Tanzania ambao wanahitaji kuandaliwa kwa soko hilo nchini na nje ya nchi.
Alisema Kampuni ya Vuvuzela imejitolea kusaidia wasanii wa vichekesho nchini na kuwafundisha namna watakavyoweza kuendeleza fani hiyo kazi iliyoanza miaka minne iliyopita kampuni ilipoanzishwa.
Bukuku alisema kila mwisho wa mwezi kuna onesho maalum ambalo hutumika kuonesha vipaji vya wasanii wa vichekesho na jinsi msanii anavyoweza kutawala jukwaa kuwaburudisha watazamaji.
Alisema kampuni yake inatarajia kufanya maonesho kama hayo mikoa mbalimbali ya Tanzania kuibua wasanii wengine wenye uwezio katika fani hiyo.
Mkurugenzi Bukuku alisema katika onesho la karibuni Watanzania walikongwa nyoyo zao pale wasanii wa Tanzania washirikiana na wasanii wa vichekesho kutoka Kenya ambaye ni Mdomo Baggy na Dick Omondi kutoka Uganda anayejulikana kama Uncle Bob kufanya onesho kali nchini.
Bukuku aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia kufanyika kwa onesho hilo ambao ni Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA),Hoteli ya  Golden Tulip, Gazeti la Mwananchi Communications, Clouds Media Group, Ultimate security, Simu TV, Prime Advertising, Dar insites, Advertising Dar, Bongo 5, Eventlites, Hugo Domingo na Michuzi Blog.
===============================================================

MBUNGE MGIMWA APIGANIA UMEME KALENGA ,WANANCHI WAKE WAMPONGEZA

Mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwa katika usafiri wa Baiskeli  kutembelea wananchi  wake
……………………………………………………………………………………….
Na Kikosi kazi  cha   matukiodaimablog Dodoma na Iringa 
MBUNGE
wa Kalenga Godfrey Mgimwa (CCM) ameiomba Serikali kupeleka umeme katika
vijiji vilivyopitiwa na umeme huku vyenyewe vikikosa Nishati hiyo.
Alitoa ombi hilo wakati akiuliza swali la nyongeza Bungeni ,Mgimwa alivitaja
vijiji vilivyopitiwa na umeme ni Kipela kata ya Nzihi,Wenda kata ya Mseke , Tagamenda kata ya Luhota,Stand ya Mbuzi na Migori kata ya Maguliwa.
Pia Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inawaambia nini wananchi wa Vitongoji vya Majengo Mapya   ,Ilala ,godown A na B kata ya Magulilwa ambayo havina nguzo za kutosha.
Akijibu Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga aliwataka wananchi
hao kutokuwa na wasiwasi na kusema nguzo zitasambazwa katika maeneo yote.
Vile vile alisema,Serikali inachukua takwimu ya vijiji vyote ambavyo vimepitiwa na  umeme wakati vyenyewe havina ili navyo vipate Nishati hiyo.
Katika swali la msingi Mbunge huyo alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka
umeme katika jimbo la Kalenga kata za Lumuli,Kiwelo ( Kiwele),Ulanda na
Magulilwa ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuongeza kasi ya maendeleo.
 Nguzo  za umeme zikiwa tayari  kata ya Mgama Akijibu Kitwanga alisema,kata hizo zimewekwa kwenye utekelezaji wa Mradi
Kabambe wa Umeme vijijini awamu ya pili wa kusambaza umeme  vijijini
kupitia ufadhili wa mfuko wa Nishati Vijijini ( REF).
Alisema kazi za mradi huo zinajumuisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa
kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 37 .7 ,ujenzi wa njia ya umeme
msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 26.
Mbunge Mgimwa  wa wa nne katikati akikagua mradi wa umeme kata ya Mgama
Kazi zingine ni ufungaji we Transfoma 12 ,transfoma moja ya kVA 25 ,Transfoma nane za kVA 50 ,Transfoma kVA 100 na mbili za kVA 200 ambapo jumla ya wateja wa awali wapatao 829 wataunganishiwa umeme.
Alisema mradi huo utagharimu kiasi cha sh.bilioni 2.0 na utekelezaji wa mradi
unatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 2015 huku mkandarasi wa kazi hiyo akiwa ni kampuni ya M/S. Sengerema Engineering Group ya Tanzania.
Kwa upande wao  wakazi wa  Magulilwa na  Kiwere na Ulanda  wamempongeza  mbunge   huyo  kwa  jitihada  zake za  kupigania maendeleo ya  jimbo la Kalenga  likiwemo suala la umeme katika maeneo yao.
Wana CCM Kalenga   wakimpongeza  mbunge  wao Godfrey Mgimwa
Akizungumza na mtandao  huu John Kibiki  kutoka kata ya  Magulilwa  alisema  kuwa wananchi  wa  eneo  hilo  wamefarijika  zaidi na kasi ya  mbunge  wao katika kupigania kata  hiyo  kuwa na umeme na kuwa kwa  kufanya hivyo  kutaongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wa kata  hiyo.
Huku Anna Sanga mkazi  wa  Kiwere  alisema  kuwa  uwajibikaji wa mbunge  wao ndio ambao  umeendelea  kuwafanya  wana Kalenga   kutoka kimaendeleo na  kuwa  wao  walikuwa hawanajiona kama bado hawajapata  uhuru  kutokana na kukosa  umeme  toka nchi ipate  uhuru wake mwaka 1961.

No comments:

Post a Comment