Kampuni ya ndege ya fastjet, 
ambayo ni Kampuni yenye gharama nafuu kote Afrika, imeadhimisha miaka 
miwili ya kutoa usafiri wa anga barani Africa.
Fastjet ilianza biashara ya 
usafiri wa anga hapa Tanzania tarehe 29 Novemba 2012, ikifanya safari 
zake kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro na Mwanza kupitia ndege 
yake aina ya A319.
Tangu wakati huo, Fastjet imepanua
 wigo wa mtandao wake nchini Tanzania pamoja na kuanzishwa kwa njia yake
 ya tatu kwenda Mbeya. Kwa sasa safari za Kimataifa za ndege hii ni 
pamoja na safari ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika ya 
Kusini, Lusaka nchini Zambia, Harare nchini Zimbabwe na Entebbe nchini 
Uganda.
Hadi sasa, ndege imeshasafirisha zaidi ya abiria 870,000 katika 
safari zake 8,200 ilizofanya zenye umbali wa takribani kilomita milioni 
6.5 – ambapo utendaji wake kwa ujumla umevutia kwa asilimia 90 kwa mwaka
 2014 kwa kuwa usafiri wenye uhakika na wa kuzingatia muda. Kampuni 
imejijengea kuwa ni ya uhakika, kuaminika na ya usafiri wenye gharama 
nafuu.
Nauli za Fastjet katika safari za 
ndani ya nchi hapa Tanzania zinaanzia dola za kimarekani 20 kwa safari 
moja, na nauli za kimataifa gharama ni ndogo kuanzia dola 50 kwa safari 
moja, zote ukiondoa kodi ya uwanja wa ndege na kodi ya serikali. Nauli 
hizi nafuu zimeifanya kampuni hii kutajwa kuwa ni yenye gharama nafuu 
kwa Afrika na ya tano kidunia kwenye unafuu wa bei ukilinganisha na 
makampuni mengine kupitia tovuti ya makampuni ya ndege, 
WhichAirline.com.
Fasjet inaamini unafuu wake wa bei
 unafanya safari za anga kupatikana kwa wingi kwa Waafrika wengi zaidi. 
Usemi huu ulihakikiwa kupitia utafiti uliofanywa na Fastjet muda mfupi 
baada ya uzinduzi wake, ambao ulionyesha kuwa asilimia 38 ya abiria wake
 walikuwa wanasafiri kwa mara yao ya kwanza ambapo kabla hawakuwa na 
uwezo wa kusafiri kwa anga.
 “Usafiri wa anga wenye gharama 
nafuu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi katika Afrika- hasa katika sekta ya
 biashara na utalii,” amesema Jimmy Kibati, ambaye ni Meneja mkuu wa 
kampuni ya Fastjet kwa Afrika Mashariki. “Hata kama kuna ndege zilizopo 
zinazounganisha majiji miwili, kwa kawaida ndege huwa inahusisha angalau
 kituo kimoja cha kusimama. Hivyo, nauli kubwa inayotozwa na mashirika 
ya ndege kwenye safari za njia hizi huwatenga wananchi wengi kufurahia 
urahisi na uokoaji muda unaotokana na faida ya kusafiri na ndege.”
Kulingana na Kibati, Fasjet 
imepiga hatua kubwa katika miaka hii miwili, licha ya changamoto ambazo 
kampuni imekuwa ikikabiliana nazo.
“Licha ya changamoto kubwa za 
udhibiti tulizokutana nazo wakati tunaanza upanuzi wa safari za 
kimataifa, serikali ya Tanzania imekuwa ikitutia moyo sana, kwa sababu 
hiyo tunawashukuru sana,” aliongeza Kibati. “Hii inatufanya tuwe na 
mtazamo chanya juu ya siku zijazo, pamoja na maoni yetu kwamba ukuaji wa
 uchumi katika Tanzania utaendelea, ukiendeshwa na tabaka la kati 
linaloibuka, na kuongezeka kwa viwango vya mapato ya hiari, ukuaji 
mkubwa katika ujasiriamali na uboreshwaji wa miundo mbinu ya uwekezaji.
Kibati pia alitoa maoni juu ya 
umuhimu wa kuwa na kitovu cha usafiri wa anga katika mji wa kibiashara 
wa Tanzania. “Dar es Salaam itaendelea kukua na kuwa kitovu cha viwanda 
na biashara katika Afrika na dunia kwa ujumla, hii inasababishwa na 
nafasi yake ya kuwa kama lango la Afrika Mashariki, maendeleo ya mafuta 
na akiba ya gesi na kuwa na miundo mbinu bora ya uwekezaji,”
Kuhusiana na usafiri wa anga kwa 
bei nafuu katika bara zima, Kibati alielezea, “Tunaamini kwamba kuna 
umuhimu mkubwa wa kuwa mfano wa ndege zenye gharama nafuu katika Afrika.
 Tumedhamiria kufanya kazi pamoja na serikali katika bara zima ili 
kukuza faida ya ushindani katika sekta ya anga. Hii itasababisha nauli 
ziwe nafuu kwa abiria. “
Kampuni ya Fasjet inaendelea kupanuka katika bara la Afrika pamoja na hivi karibuni kutangaza kwamba operesheni take mpya

No comments:
Post a Comment