WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI WAPEWA SEMINA YA UHIFADHI WA MAZINGIRA.
Meneja
  Uhifadhi wa Shirika la Utunzaji wa Mazingira WWF Tanzania, Dr. Amani 
Ngusaru ,akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo 
vya habari mbalimbali katika semina ilioandaliwa na (WWF) iliofanyika 
Disemba 2-3, 2014 mkoani Morogoro juu ya utunzaji wa mazingira ili 
kuleta uwiano sawa wa rasilimali zinazopatikana maeneo mbalimbali 
nchini. 
Mkurugenzi
 wa  Shirika la Utunzaji wa Mazingira WWF Tanzania Bw. Bell’Aube 
Houinato akielezea malengo ya Shirika hilo, ambayo pamoja na mambo 
mengine ni kuhakikisha ulinzi wa viumbe hai na misitu izingatiwe ili 
kulinda mazingira na  kuinua uchumi wa taifa. 
Kiongozi
 wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira WWF, CEA (Coastal East Africa 
Global Initiative Leader), Peter Scheren akifafanua jambo katika mkutano
 wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika utendaji wao kazi katika
 uhifadhi wa mazingira. Kwamba kuwepo na ushirikiano katika utunzaji wa 
mazingira ili kuleta uwiano sawa na rasilimali ambazo zinapatika katika 
maeneo husika. 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Bw.Magese Bulayi akisisitiza jambo kuhusiana uvuvi haramu wakati wa semina hiyo. 
Mtaalam
 wa Maendeleo ya Uhifadi kutoka Shirika la WWF Tanzania, Prof.Hussein 
Sosovele akiwakilisha mada yake wakati wa semina hiyo ambapo amesema 
kuwa kutoka na elimu inayotolewa na WWF katika maeneo mbalimbali hapa 
nchini, baadhi ya jamii zimeshatambua umuhimu wa hifadhi katika 
maeneoyao.  “Mapato hayo ni kiwango kikubwa mno, kwa kuwa yanasaidia 
kusukumamiradi ya maendeleo kakika kijiji husika. Ingawa kuna changamoto
 zahapa na pale lakini tunaamini haya ni mafanikio na kila mmoja 
wetuanapaswa kushiriki katika utunzaji wa mazingira,” alisema Profesa 
Sosovele. 
Waandishi wa habari wakichangia maada mbalimbali. 
 
Wahariri
 na waandishi wa habari wakiwa katika majadiliano ya namna ya 
kukabiliana uvuvi haramu katika mwambao wa bahari ya Hindi. 
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment