.Naibu
 Waziri wa Fedha,Adam Malima(kushoto)akisalimiana  na Makamu Mwenyekiti 
wa Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Ahmed Kilima alipowasili
 jijini Arusha kufungua mkutano wa Siku mbili wa Wataalamu wa Ugavi 
nchini,wengine ni kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,Clemence Tesha
 na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dk Hellen Bandio. 
Naibu
 Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa  Bodi ya Wataalamu 
wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa  Siku mbili unaofanyika 
kwenye kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha
Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha. 
Naibu
 Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa  Siku
 mbili  wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)  unaofanyika 
kwenye kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha. 
Mkurugenzi
 Mtendaji wa  Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence  
Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba 
nzuri. 
Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha.
…………………………………………………………………………………….
Mwandishi wetu,Arusha
 WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya 
Wataalam wa  Ugavi na Manunuzi nchni  (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa 
tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na 
kuwataka waajiri kuacha mara moja  kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya 
kazi hizo
 Naibu Waziri wa Fedha,Adam 
Malima ametoa kauli hiyo leo  wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka 
wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha
 ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.
 Amesema katika bajeti ya mwaka 
2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia 
65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma 
mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti 
mapato ya serikali yasitumike vibaya.
 Awali  Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
 Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo “Thamani 
halisi ya fedha  za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha serikali inapata 
huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.
 Amesema Bodi hiyo imezalisha 
wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali ambayo ni sawa na 
asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri watumishi 
wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
No comments:
Post a Comment