Mbunge wa jimbo la Mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa  
Mbunge
 wa jimbo la Mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili 
na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa na mkuu wa wilaya wa mufindi.
Na fredy mgunda Iringa.
Vijiji 31 vilivyopo mufundi 
kaskazini mkoani Iringa vinatarajia kupokea umeme na tayari baadhi ya 
vijiji vipo katika hatua ya mwisho ya kufunga vikombe kwaajili ya kuanza
 kuvuta nyaya.
Akizungumza na mwandishi wetu 
katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini ambae pia ni naibu waziri
 wa maliasili na utalii Babtist Mdende amesema kuwa, vijiji 
vinavyotarajia kupata umeme safari hii ni vile vijiji vilivyopo tarafa 
ya sadani,ifwagi na kibengu.
“vijiji hivyo ni mapogoro, 
igomaa,kibada,ndolezi na vengine kama ugesa,vikula,ilasa na kipanga 
ambavyo upimaji bado unaendelea kwaajili ya kusimika nguzo, 
“kunabaadhi ya vijiji vipo 
katika hatua ya awali ya kusimamisha nguzo ikiwepo kijiji cha Isalavanu 
ambacho mradi wake wa umeme unashughulikiwa na TANESCO wilaya ya 
mufindi”, alisema Mdende.
Aidha Mdende ameeleza kuwa kwa 
wale watakao ingazwa kwa mara ya kwanza yaani watu wa kwanza wakati wa 
kuzindua mladi wa umeme wataingiziwa kwa gharama ya shilingi elfu 30
No comments:
Post a Comment