![]()  | 
| Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza na waandishi wa habari | 
Mwenyekiti
 wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo amempa siku saba kocha 
wa timu ya Mwadui  Jamhuri  Kihwelo  amuomba radhi kwa kile alichodai 
kuwa ametoa lawama zisizo za kweli dhidi yake kupitia vyombo vya habari.
Akizungumza
 na waandishi wa habari Kitumbo alisema amesikitishwa na taarifa 
alizozitoa kocha huyo dhidi yake zinazomhusisha kuwa amekuwa akileta 
vurugu katika michuano ya ligi daraja la kwanza kwa madai kwamba amekuwa
 akifanya fitina kupitia kuwahonga  fedha  waamuzi ili timu mbili za 
mkoa wa Tabora Rhino Rangers na Polisi Tabora ziweze kufanikiwa kuingia 
ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
 Kitumbo
 kupitia vyombo vya habari amemtaka kocha huyo Jamhuri Kihwelo 
kuthibitisha madai yake vinginevyo atamchukulia hatua zinazostahili kwa 
kile alichodai kuwa kiongozi huyo wa timu ya Mwadui amesema uongo.
 Alisema
 kitendo cha kocha huyo kuelezea tuhuma dhidi yake kupitia Star Tv 
katika kipindi TUONGEE ASUBUHI ambazo alidai kuwa zimemharibia mwenendo 
wa kazi zake si za kweli na kuwataka watanzania kutomwamini kocha huyo 
ambaye si mkweli.
 “Naomba
 kocha Jamhuri Kihwelo aniombe radhi kwa muda wa siku saba na ninampa 
siku saba kuanzia leo tarehe 3 Desemba 2014 na kama asipofanya hivyo 
asinilaumu kwa hatua nitakazozichukua,najua kuwa TFF wananisikia kwa 
haya ninayoyasema nitamfikisha kwenye vyombo vyenye mamlaka ya soka 
viweze kumshughulikia”alisema Kitumbo.

No comments:
Post a Comment