Muongozaji
 wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi, Jordan Riber akizungumza katika 
uzinduzi wa tamthilia hiyo Sehemu ya pili  kwenye ukumbi wa Cinemax 
Century jijini Dar es salaam.
MC wa shughuli ya uzinduzi wa Siri ya Mtungi 2, Ambi Lusekelo akimtambulisha muigizaji nyota wa tamthilia hiyo, Cheche
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo Katikati na wadau wa Filamu Tanzania waliohudhuria
 katika uzinduzi huo  wakifuatikia hotuba bali mbali zilizotolewa wakati
 wa uzinduzi wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu ya pili.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo Katikati na wadau wa Filamu Tanzania waliohudhuria
 katika uzinduzi huo  wakifuatikia hotuba bali mbali zilizotolewa wakati
 wa uzinduzi wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu ya pili.
Maofisa
 kutoka kampuni ya John Hopkins University For Communication Programs 
(JHU CCP) ambao moja wa wadhamini wa tamthilia hiyo katika picha ya 
pamoja.
Le
 Mutuz akiwa na mmoja wa waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu 
ya pili Richa Adhia, Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda na 
Muigizaji mkongwe nchini, Mwita nao walikuwepo katika uzinduzi huo
Waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya uzinduzi rasmi kwenye ukumbi wa Cinemax Century
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Bodi ya 
Filamu Tanzania imewataka waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano wa 
waandaaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Shirika Lisilo la Kiserikali 
(NGO ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) kwa kutoa
 filamu yenye mafundisho mbali ya kuburudisha.
Kauli hiyo 
imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo 
kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice Sumari kwenye ukumbi wa Cinemax 
Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha wadau wa fani hiyo, 
wadhamini na waandaaji.
Sumari 
alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya Mtungi Msimu wa Pili mbali ya 
kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania wengi, pia imeleta 
changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.
“Filamu 
imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani 
hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta katika jamii filamu yenye ubora huu,
 naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema  Sumari.
“Filamu hiyo 
ina ubora  wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa matukio wa kipekee na
 kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo ukianza kuangalia, 
hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,” alisema.
Afisa kutoka 
Taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo alisema 
kuwa wanajisikia furaha kudhamini tamthilia hiyo ambayo imezungumzia 
maisha halisi ya Mtanzania.
Bodipo 
alisema kuwa alisema kuwa tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na 
ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki 
katika masuala ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Matukio 
mengi katika tamthilia hii yana akisi taswira ya kweli katika jamii na 
na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo halisi kutokana na changamoto 
mbalimbali,” alisema Bodipo.
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na kufichua kilichopo katika mtungini.
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin alisema
 kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the 
John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP) 
ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya 
Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na
 MFDI.
Mwisho….
.




No comments:
Post a Comment