Waziri
 wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa 
akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za 
utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA 
uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000 
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango 
huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea 
kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu
Tanzania
 imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini 
mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa 
wote (EFA)
Akihutubia
 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wote wa elimu , 
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru 
Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani imeweza kukaribia kufikia 
malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala la wastani wa waalimu kwa
 wanafunzi.
Amesema
 kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi 
47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu 
mmoja kwa wanafunzi 27.
Mafanikio
 mengine yaliyopatikana chini ya mpango huo ni kuboresha wastani wa 
wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania Bara wastani umetoka kuwa 
wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi 65 huku Zanzibar wastani 
ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
Mkurugenzi
 Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi 
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza wakati wa 
mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto 
zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu
 kwa Wote –EFA ulioshirikisha wadau wote wa sekta ya elimu uliofanyika 
jijini Dar Es Salaam. Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuiandaa 
Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mashauriano ya kiserikali 
baina nchi mbalimbali na kuhakikisha wadau wakuu wa elimu kitaifa 
wanapata taarifa juu ya mapendekezo ya agenda zitakazoanza mwaka 2015.
Awali
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia 
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema 
ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo
 Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati 
ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.
Bi. 
Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na 
Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo 
kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na 
kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha , 
wadau, usimamizi na uwajibikaji.
Katika
 mkutano huo imeelezwa kwa sasa hakuna tatizo la uwiano wa wanafunzi wa 
kike na wa kiume kwa kuwa jinsia zote zipo darasani katika uwiano 
unaoridhisha unaokaribia wastani wa 50/50, lakini pia kigezo kingine ni 
uwiano wa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari ambapo bado 
kumeonyesha kuwa na mapungufu hivyo kazi ya ziada inahitajika.
Mkutano
 huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa 
nchi wahusika kujitathimini zimefikia wapi katika utekelezaji wa malengo
 waliyojiweke ya Mpango wa Elimu kwa Wote-EFA kwa kipindi cha mwaka 2000
 hadi 2015 na kujiwekea mikakati mipya.
Pichani juu na chini ni sehemu
 ya wadau wa elimu kutoka bara na visiwani wakifuatilia hotuba za 
viongozi wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na 
changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa 
Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA.
Kamishna
 wa Elimu kutoka Wizarani, Prof. Eustella Bhalalusesa (wa pili kushoto) 
akitoa maoni juu changamoto zinazolikabili taifa katika kuleta uwiano 
kwenye ya sekta elimu.
Mkurugenzi
 Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi 
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akishea uzoefu wake katika 
utekelezaji wa malengo ya EFA baina ya Tanzania na nchi zingine za 
Afrika.
Naibu
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Maalim 
Abdallah M. Abdallah (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa 
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na 
Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mkutano huo. Kushoto
 ni Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru
 Kawambwa.
Waziri
 wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa
 akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa 
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira 
Rodrigues baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Mkurugenzi
 wa ofisi ya elimu kutoka Shirika la USAID, Bw. David Bruns (kushoto) 
akibadilishana mawazo na Waziri Kawambwa (katikati) na Bi. Zulmira 
Rodrigues.
Afisa
 Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko akiteta jambo na
 Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta.
Waziri
 wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa,
 akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na nafasi
 ya Tanzania ilipofikia tangu 2000-2015 katika utelekezaji wa malengo ya
 EFA.
Afisa
 mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akizungumza 
na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa mkutano huo baina ya UNESCO na 
Wizara katika kutathmini utelekezaji wa malengo ya EFA katika kipindi 
cha miaka 15 na kutoa nafasi ya kujipanga kwa awamu nyingine itakayoanza
 2015-2030.
















No comments:
Post a Comment