MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA 
MELANIA RICHARD (60) MKAZI KIJIJI CHA KAMFICHENI ANASHIKILIWA NA JESHI 
LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA 
LITA 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 
04.12.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA 
KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA 
CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, 
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MRISHO
 RAMADHAN (22) MKAZI AIRPORT ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA 
MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 01 SAWA NA UZITO WA GRAM 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 
04.12.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MANGA, KATA YA
 MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
 MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA 
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII 
KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI/BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI 
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

No comments:
Post a Comment