Mkurugenzi
 wa Utetezi na Maboresho ya Sera wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
 (LHRC), Halord Sungusia (katikati), akizungumza katika mkutano na 
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tathmini ya 
mwenendo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika 
kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow. Kushoto 
ni Ofisa Mipango Dawati la Uangalizi wa Serikali wa LHRC, Hussein Sengu 
na Wakili, Hamisi Mkindi. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
 Wakili, Hamisi Mkindi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema Mahakama isitumiwe kama kinga ya kufanya uhalifu.
Hayo 
yamebainishwa Dar es saalam leo na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho ya
 Sera  wa LHRC, Halord Sungusia wakati akizungumza na wanahabari 
alipokuwa akitoa tathmini ya mwenendo wa Bunge la Tanzania katika 
kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
“Mahakama
 ni taasisi kuu kitaifa ya kutoa haki kwa wananchi wote lakini isitumiwe
 na mtu au taasisi yoyote kama kinga yake ya kufanya uhalifu” alisema 
Sungusia.
Aidha 
alibainisha kuwa katiba ya sasa inatoa mianya mingi ya kutozingatiwa kwa
 miiko ya uongozi hasa baada ya kufutwa kwa azimio la Arusha na rasimu 
ya pili ya katiba iliweka msingi huu wa maadili ya uongozi kwa upana na 
kwa msisitizo.
Sungusia 
aliongeza kuwa nchi haitokuwa salama kama katiba inayopendekezwa 
itapitishwa kama ilivyo kuwa  kwani inayopendekezwa haizungumzii kwa 
mapana maadili na miiko ya viongozi wa umma, haiweki misingi bora ya 
uwajibikaji na kusimamia dhamana ya uongozi na kanuni za uongozi wa 
umma.
Katika 
hatua nyingine LHRC kimetaka wale wote ambao watabainika katika sakata 
la utoaji wa fedha katika akaunti hiyo wachukuliwe hatua kali za 
kisheria.
No comments:
Post a Comment