Waziri
 wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye 
masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya 
Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la 
Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
Waziri
 wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa 
mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba
 ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi 
wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas. 
Baadhi
 ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na 
wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha 
Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia 
Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu
 kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)
…………………………………………………………………….
Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania imesainiana mkataba wa mkopo wa zaidi ya 
shilingi bilioni 45.21 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la 
kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na 
ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.
Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa 
Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi 
wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas
Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada 
alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na 
Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya 
za Same na Mwanga na shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa 
barabara Pemba, visiwani Zanzibar.
Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa 
jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la
 maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika 
visiwa vya Pemba.
Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za 
Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo 
Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha
 iliyobakia.
Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia 
kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida 
kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa 
maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha 
uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali 
badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia 
Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha 
kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono 
Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano 
mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo. 
Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya 
watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment