Mratibu
 wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) Suleiman 
Salum  Ali  akieleza mafanikio  ya mafunzo hayo  yaliyofanyika Hoteli ya
 Double Tree Nungwi, wa kwanza (kulia) ni Profesa Kristin Braa kutoka 
Chuo Kikuu cha Oslo ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo kwa kushirikiana 
 na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar. (kati) ni 
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliefunga mafunzo hayo. (Picha
 na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar) 
Naibu
 Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti mmoja ya
 washiriki wa mafunzo ya D.H.I.S  Osama Al Zubair  kutoka Sudan wakati 
wa kufunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi, Kaskazini 
Unguja.  
Mgeni
 rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya D.H.I.S Mahmoud Thabit Kombo 
akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo kutoka Nchi za Afrika, Marekani, 
Ujerumani na Mashirika wahisani katika Hoteli ya Double Tree Nungwi. 
Washiriki
 wa mafunzo hayo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud 
Thabit Kombo alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku 10 yaliyofanyika 
Hoteli ya Double Tree Nungwi. 
Mratibu
 wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya Suleiman Salum Ali 
akizungumza na waandishi wa Habari walioshiriki ufungaji wa mafunzo hayo
 katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
Picha
 ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za 
Afya (D.H.I.S) wakiwa na mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo Naibu 
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
 (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar).
No comments:
Post a Comment