TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 5, 2014

Mtandao wa Kuchepuka wa Zari the Lady Boss ni Kiboko Diamond ni wa 13


diamond na zari the boss

 Ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha kila kukicha, mrembo tajiri mwenye maskani yake nchi jirani ya Uganda na Afrika Kusini, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, anadaiwa kuwa na mtungo mrefu wa wanaume ambapo kama ni kweli anatoka na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ basi jamaa huyo atakuwa anashika nambari 13.
Kwa mujibu wa jarida la linalodili na habari za showbiz (biashara ya shoo) la E-Vibe la nchini Uganda la hivi karibuni, Zari ambaye wikiendi iliyopita alimng’arisha Diamond katika zulia jekundu kwenye Tuzo za Channel O (Choamva) zilizofanyika Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’, anadaiwa kuwa ‘klozi’ na idadi hiyo ndefu ya wanaume.
Jarida hilo lilieleza kwamba ndani ya kipindi cha miaka 14 baada ya kutimiza umri wa mtu mzima wa miaka 18, Zari mwenye umri wa miaka 32 sasa, ameshajiachia na wanaume wa kada mbalimbali wakiwemo vigogo serikalini, wafanyabiashara, mastaa wa tasnia mbalimbali na hata vijana wadogo.

MABUSU

Kabla ya Diamond, picha za Zari zilivuja akiwa anabusiana kwa hisia na mwanaume, Farouk Sempala anayesifika kwa dili za mjini. Mara nyingi, Zari amekuwa akishangaza watu na kuacha maswali kuwa nini huwa kinamsukuma kumzoea mwanaume haraka na kuingia naye kwenye urafiki?
Kwa mujibu wa jarida hilo, kuna mtandao maalum wa kundi la watu uliundwa kwa ajili ya kufuatilia nyenendo za Zari katika sekta ya mapenzi ndipo data zikamwagwa.

MUMEWE

Jarida hilo liliweka wazi baadhi ya wanaume walioko kwenye listi hiyo kuwa ni pamoja na mumewe, Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu kabla ya kumwagana mwaka jana bila talaka.

STAA WA KIKAPU

Mwingine anayetajwa kwenye listi hiyo ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda. Hata hivyo naye hakudumu naye.

MIKONONI MWA MTOTO WA MJINI

Lilidai kwamba baada ya Zari kuondoka kwa mumewe Semwanga na  kumwacha na watoto nchini Afrika Kusini, mwanadada huyo aliangukia kwenye penzi la mtoto wa mjini nchini Uganda, Farouk Sempala ambaye aliposikia tetesi kuwa anatoka na Diamond ndipo akatangaza kuachana naye.

WENGINE

Wengine waliotajwa katika jarida hilo ni pamoja na Jenerali Jeje Odong, wasanii wa muziki, Mozed Radio na  Weasel. Katika listi hiyo ndefu pia wamo Aziz Azion, Isaiah, Robert Ogwal a.k.a Rasta Rob, Exodus, Dj Shiru, mfanyabiashara wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond.

DIAMOND NA ZARI

Awali walianza kama utani ikisemekana kwamba kuna ‘projekti’ wanaifanya kwa kuwa wote ni mastaa wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo, kwa kadiri siku zilivyosonga mambo yakazidi kuwa hadharani na sasa kila kitu kipo wazi na kwamba kama hujui kusoma, angalia picha wanavyojiachia kama baba na mama.
Wakiwa nchini Afrika Kusini wikiendi iliyopita, Zari anadaiwa kujitambulisha rasmi kwa mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambapo walikuwa beneti hadi watu wakawa wanamsifia Zari kwa kujua umuhimu wa mama mkwe na kumhudumia vizuri.

ZARI ANASEMAJE?

Kwa kuwa kila tukimuuliza Diamond ana uhusiano gani na Zari amekuwa akichenga, kwa upande wa mwanadada huyo amekuwa akichekacheka na kudai wapo kikazi zaidi huku akimsifia jamaa huyo kwenye mitandao ya kijamii.

TATIZO UMRI

Kwa mujibu wa makabrasha ya gazeti hili, Diamond ana umri wa miaka 25 wakati Zari ana miaka 32 hivyo amemzidi kwa miaka 7 hivyo kuonekana ‘anambemenda’ Mbongo Fleva huyo.

WATOTO

Mwanadada Zari ana watoto watatu aliozaa na mumewe, Semwanga huku Diamond akiwa hana hata wa kusingiziwa (kama yupo mwenye mtoto wa Diamond ajitokeze).

WEMA AMWITA DIAMOND KAKA

Tofauti na walivyozoea kuitana ‘Baby’, siku hizi upepo umebadilika kwani aliyekuwa mwandani wa Diamond, Wema Isaa Sepetu amekuwa akimwita jamaa huyo kaka, siku alipompongeza kwa ushindi huo na hivyo kuibua maswali ya kufa mtu.

WABONGO WATAKUNYIMA MSOSI SI MANENO

Wakizungumzia uhusiano wa Diamond na Zari, Wabongo waliozungumza na gazeti hili walionekana kugawanyika.
Wapo waliodai kuwa mwanamama huyo haendani na Diamond kwa kuwa umri umeenda lakini wapo wanamsifia jamaa huyo kwa kufanikiwa kumnasa Zari mwenye umbo bomba, mrembo ambaye fedha zimemtembelea.

No comments:

Post a Comment