Mwenyekiti
 wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim 
Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa 
wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya 
kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano 
hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa 
hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania 
(Bloggers).  Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, 
Othman Maulid.
 Katibu
 Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha 
(kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya 
rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati,  Henry Mdimu.
 Wajumbe wa kamati wakipitia rasimu hiyo. Kulia ni William Malecela na Mariam Ndabaganga.
 Mwenyekiti
 wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim 
Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa 
wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya 
kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano 
hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa 
hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania 
(Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa 
Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha,  Henry Mdimu 
(Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Longue, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 
 
 
 
 
 
 
Na Dotto Mwaibale,
WAJUMBE
 wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers) 
wameanza vikao vyao kujadili rasimu ya katiba ya umoja huo kabla ya 
kufanya usajili wa chama chao kitakacho waunganisha wamiliki na 
waendeshaji wa mitandao hiyo Tanzania.
Akizungumza
 leo katika vikao hivyo vinavyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti 
wa Muda wa Kamati ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania, Joachim 
Mushi amesema wajumbe waliokutana ni wawakilishi wa wamiliki wa mitandao
 hiyo kutoka makundi mbalimbali ya waendeshaji hao wa mitandao ya jamii 
nchini.
Alisema
 pamoja na mambo mengine wajumbe hao wanatarajia kufanya majadiliano 
baada ya kuipitia rasimu ya Katiba ikiwa ni kuelekea mchakato wa kupata 
Katiba ya Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania. Alisema 
masuala mengine ambayo yataongoza mjadala huo ni pamoja na kuangalia 
muundo wa chama, uendeshaji wake, maadili ya chama kwa wanachama katika 
utekelezaji kazi zao.
“Kikao
 hiki kinashirikisha wajumbe wa kamati ambao ni wawakilishi wa makundi 
mbalimbali ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya jamii Tanzania na 
kazi kubwa ambayo wataifanya leo kwa pamoja ni kupitia rasimu ya uumoja 
wetu. Wajumbe wote walikabidhiwa rasimu hii wiki mbili zilizopita 
kuipitia wenyewe kabla ya kukutaka katika majadiliano ya leo,” alisema 
Mwenyekiti wa Muda, Mushi.
Aidha
 aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mchango wake wa 
dhati wa kuwaunga mkono Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania hasa 
katika kipindi hiki cha mchakato kuelekea uundwaji wa chama chao. 
Miongoni
 mwa wajumbe wa kamati hiyo ya muda waliokutana ni pamoja Shamim Mwasha 
(Katibu Msaidizi) Khadija Kalili (Katibu), Joachim Mushi (Mwenyekiti), 
Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe), William Malecela 
(Mjumbe), Othman Maulid (Mjumbe-Zanzibar) na Francis Godwin (Makamu 
Mwenyekiti – Iringa).
Mkutano
 wa mafunzo wa idadi kubwa ya wawakilishi wa wamiliki wa mitandao ya 
kijamii nchini (Bloggers) uliofanyika Novemba 11, 2014 jijini Dar es 
Salaam ulioitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania uliibua uundwaji 
wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania chini, 
ambapo kamati hiyo ilipewa jukumu la kupitia rasimu kabla ya 
kushughulikia usajili wa chama cha jumuia hiyo.
No comments:
Post a Comment