Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’
 Lady Jaydee akisoma gazeti la Staa Spoti.
 Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Jambo Leo, Frank Balile (kulia), akimuelekeza jambo Lady Jaydee wakati akimuonesha gazeti hilo.
Mwanadada
 anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 
‘Lady Jaydee’ akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, 
alipotembelea chumba cha habari Dar es Salaam jana.
Dotto Mwaibale
MWANADADA
 anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 
‘Lady Jaydee’ amesema kamwe atarajii kujiingiza katika masula ya siasa 
kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.
Kauli 
hiyo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti la 
Jambo Leo Dar es Salaam jana, baada ya kutembelea chumba cha habari cha 
gazeti hilo katika Jengo la Hifadhi House katika makutano ya Barabara za
 Azikiwe na Samora.
“Binafsi 
sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na 
hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao.
Alisema 
anafurahi kufanya mziki na wala hajuti kwa kuwa unamuongezea kipato 
kikubwa ni kutunga nyimbo zenye mahudhui na mvuto na kwa wakati husika.
Baadhi ya
 wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye 
ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa J, Khadija Shabani ‘Keisha’ 
Ummy Wenslaus ‘Dokii, na wengine kama Fullgence ‘Mwanacotide’ ambaye 
yupo Chadema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment