Bw.
 Peragius  Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata  
GPA 4.91 akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE 
Prof.Emanuel Mjema.
Bi.
 May Issa  mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa 
manunuzi  na kupata  GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu
 wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
Kwa
 kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara 
(CBE)  wanafunzi hawa  kutoka kampasi ya Dodoma  wameweza kupata ufaulu 
mkubwa katika masomo yao.
Bi. May Issa  Mwanafunzi 
 aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa  Manunuzi  katika 
mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 
ametangazwa  kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata
 GPA ya  4.92. ambapo  aliweza kupata alama  A  28 , alama  B+ tatu  na 
 alama  B  moja  kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  
Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na  Bw. Peragius Cosmas  aliyepata GPA 
ya 4.91.
  Kwa upande  wake 
Mwanafunzi mwingine  Bw, Peragius Cosmas  aliye kuwa akisoma Shahada ya 
kwanza ya Uhasibu   yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA 
ya  4.91  ambapo aliweza kupata alama  A  29 na  alama  B+ tatu    kati 
ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  uhasibu.
 Hivi  karibuni katika Chuo
 kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  pia tulishuhudia  Msichana   Doreen 
Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa  Mhitimu bora wa Chuo Kikuu
 cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara 
kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada
 ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata 
wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia 
kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano,
 Bi.
 May  Issa akionekana mwenye furaha siku ya mahafali  ya 49 iliyofanyika
 hivi karibuni katika chuo cha Elimu ya biashara kampasi  ya Dodoma.
Bw.
 Peragius Cosmas akionekamna mwenye furaha  katika mahafali ya  49 ya  
chuo cha CBE iliyofanyika hivi karibuni katika  Chuo cha Elimu ya 
Biashara kampasi ya Dodoma.
  Rais
 mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi CBE  kampasi ya Dodoma 2013/2014 Bw. 
Remidius Emmanuel (kulia) akimpongeza  Bi. May  Issa kwa kufanya vizuri 
katika  masomo yake  kwa kipindi chote cha masomo yake.

No comments:
Post a Comment