Na Mwandishi Wetu 
KAMPUNI ya Msama Promotions imeanza rasmi kusambaza Dvd ya 
Uniongoze ya nyota wa nyimbo za injili nchini Zambia, Ephraim Sekeleti 
tangu mwezi Novemba mwaka huu.
Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Mkurugenzi wa Msama 
Promotions, Alex Msama DVD hiyo ina nyimbo nane  ambazo ameziimba katika
 lugha ya Kiswahili.
Msama alisema hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa 
muziki wa injili kutoka kwa muimbaji huyo anayetamba na kibao cha 
‘Uniongoze’ imeingia sokoni kwa kishindo kutokana na ubora wa albamu 
hiyo.
Alisema msanii huyo kutoka Zambia alijizolea umaarufu hapa 
nchini baada ya kushiriki kwenye matamasha ya Pasaka na Krismasi 
kutokana na uwezo wake wa kumiliki jukwaa pamoja na sauti yake.
Msama albamu hiyo ya Uniongoze imetayarishwa na Msama Video 
Productions na kusambazwa na Msama Promotions ambayo ina ubora wa hali 
ya juu, hivyo mashabiki na waumini mbalimbali wajitokeze kwa wingi 
kujionea kazi zilizofanywa na kampuni hizo.
Aidha Msama alijipambanua kwa kueleza kwamba inapatikaba kwenye 
maduka ya Msama yaliyopo Kariakoo mtaa wa Masasi na Msimbazi na Posta 
mtaa wa Mkwepu.
Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Uniongoze, Baraka za 
Mungu, Kidonge cha Yesu, Wewe uko, Ndani ya jina, Kuna wakati Nachoka, 
Mungu mwenyewe na Ephraim Sekeleti interview.

No comments:
Post a Comment