Rais
 wa TFF akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari 
(Hawapo pichani) kuhusiana na Kombe la Wanawake Taifa ambapo ni 
mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yaliyodhaminiwa na Kampuni ya 
Proin Promotions Ltd.
 Mkurugenzi
 wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza akizungumzia jinsi kampuni ya 
Proin Promotions Ltd ilivyoona umuhimu wa kuchangia katika kuinua soka 
la wanawake nchini na kuamua kudhamini Shindano hilo lijulikanalo kama 
Kombe la Wanawake Taifa ambalo litaanza rasmi tarehe 28 kwa mechi ya 
uzinduzi kati ya Mwanza na Mara huko Mkoani Mwanza
 Meneja
 Biashara wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF) Peter Simon 
akizungumzia juu ya ratiba ya mashindano hayo yajulikanayo kama Kombe la
 Wanawake Taifa ambapo timu za wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania 
zitashiriki katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya 
Usambazaji na utenegenezaji wa Filamu za Kitanzania ijulikanayo Kama 
Proin Promotions Ltd
Bi
 Rose Kissiwa, Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania 
akizungumzia juu ya udhamini uliotolewa na kampuni ya Proin Promotions 
Ltd katika kufanikisha Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Wanawake 
yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo uzinduzi wa Mashindano 
hayo yatafanyika Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha TImu za Mwanza na 
Mara.
Shirikisho
 la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) leo imemtambulisha rasmi 
Kampuni ya Proin Promotions Ltd kuwa mdhamini mkuu wa Mashindano ya 
Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa 
ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 28 
Disemba 2014 katika Uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza kwa 
kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.
Akizungumzia
 Udhamini huo uliotolewa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Rais wa TFF
 jamal Malinzi amesema kuwa Anawashukuru kwanza Proin Promotions Ltd kwa
 kuona umuhimu pia wa kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake hapa
 nchini kwa kudhamini mashindano ya Kombe la Wanawake Taifa ambapo 
katika mashindano hayo timu kutoka mikoa yote ya Tanzania zitashiriki na
 hatimaye kuja kupata Mshindi. Mbali na Mashindano hayo Mechi zote za 
Mashindano hayo zitarekodiwa na kuweza kurushwa katika vituo mbalimbali 
vya habari ambapo watanzania watapata nafasi ya kuwapigia kura wachezaji
 bora katika kila nafasi na kuwawezesha kushinda.
Akizungumzia
 Swala hilo Mkurugenzi Wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd, Bw Johnson 
Lukaza amesema kuwa mpaka sasa Mazungumzo bado yanaendelea na wamiliki 
wa Vituo vya Televisheni ili kuona uwezekano wa wao kurusha Mashindano 
hayo na kuwawezesha watanzania kuwapigia kura wachezaji. ameongezea kwa 
kusema kuwa Mara tu mazungumzo hayo yakimalizika na kuweza kupata nafasi
 kutoka kituo chochote cha Televisheni ambacho kitakubali kurusha 
mashindano hayo basi umma wa watanzania watatangaziwa.
Proin
 Promotions Ltd ambao  ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo ya Kombe 
la Wanawake Taifa inatoa nafasi pia kwa makampuni mengine katika kujitoa
 na kuungana nao ili kuweza kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa 
wanawake lengo likiwa ni kuboresha Timu ya Taifa ya wanawake Tanzania.
No comments:
Post a Comment