Kaimu
 Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Wapili 
kushoto) akitoa maelezo kuhusu Kiwanja cha Ndege Kigoma kwa Kiongozi wa 
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya 
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia). Wanaosikiliza ni Meneja Mradi wa 
Utanuzi wa Kiwanja cha Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha (Kushoto) na Bw. 
Julius Edward (Wapili kulia).
Meneja
 Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha 
(Kushoto) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli 
za maendeleo kiwanjani hapo.
Kaimu
 Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Aliyenyanyua 
mikono) akitoa maelezo juu ya sehemu zitakazoendelezwa kwa Timu ya 
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. 
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto)
 akiangalia tabaka za udongo uliotumika katika kujengea Kiwanja cha 
Ndege Kigoma. Anayemuonesha ni Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma,
 Bw. Joseph Nyahende (Kulia).
Meneja
 Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha 
(Wapili kulia) akionesha eneo likaloboreshwa katika Mradi wa Utanuzi wa 
Kiwanja cha Ndege cha Kigoma.
………………………………………………………………………………………
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali
 imeazimia kuanza kufanya utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ili kuweza
 kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku ya kiwanja hicho.
Azma 
imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka 
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya 
ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa 
Kigoma.
Bibi 
Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini
 ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza uwanja huo ili uwe wa kiwango kizuri 
kwa kuhudumia watumiaji wa wa kiwanja hicho.
“Kama
 munavyokumbuka Serikali katika mwaka ujao wa fedha imepanga kuendeleza 
na kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi; na 
kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika 
maeneo ya kimkakati ikiwamo Kiwanja cha Ndege cha Kigoma,” alisema.
Kwa 
mujibu wa Bibi Mwanri, uendelezaji wa Kiwanja hicho utajumuisha ujenzi 
wa jengo la abiria pamoja na miundombinu yake (maegesho ya ndege, 
maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka) na kurefusha 
barabara ya kuruka na kutua ndege.
Akiwasilisha
 taarifa ya maendeleo ya uwanja huo, Meneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja 
cha Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha alisema kuwa mpaka sasa Mamlaka ya 
Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini imekamilisha taratibu za kumpata 
mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa usalama na eneo la maegesho ya
 ndege.
“Kwa 
sasa tunaendelea na kazi ya utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa 
ajili ya kazi za ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya 
magari, na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa maegesho ya ndege 
pamoja na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege,” alisema.
Mhandisi
 Neema aliongeza kuwa wapo kwenye mchakato wa kumpata Mhandisi Mshauri 
wa kufanya usanifu wa jengo la abiria uwanjani hapo.
Naye 
Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende alisema 
kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Mamlaka ya 
Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini kwa kushirikiana na Mkoa wa Kigoma
 vimeainisha na kufanyia tathmini eneo litakalotumika kwa ajili ya kazi 
hiyo.
No comments:
Post a Comment