Katibu Mkuu wa TASWA Bw. Amir 
Mhando akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports 
Lounge wakati kamati hiyo ilipotangaza wanamichezo watakaowania tuzo ya 
mwanamichezo bora wa mwaka inayoandaliwa na Chama cha waandishi wa 
habari za michezo TASWA, kutoka kulia ni Mahmoud Zuberi Makamu 
Mwenyekiti wa kamati na katikati ni Rehure Nyaulawa Mwynekiti wa kamati 
hiyo.
…………………………………………………………………………………………….
KAMATI ya Kusimamia Tuzo za 
Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa Chama cha Waandishi wa Habari za 
Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kupitia majina 
ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo.
Tuzo itafanyika Desemba 12 mwaka
 huu ukumbi wa Diamond, Jubilee (VIP), Dar es Salaam, ambapo wanamichezo
 mbalimbali waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014 
watakabidhiwa tuzo zao.
Ni imani yetu kwamba zaidi ya 
wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo, ambapo kamati 
imejiridhisha kwamba wanaowania tuzo hiyo wanastahili kulingana na 
mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia Kamati zao za Ufundi.
Mshindi wa kila tuzo ataingia 
katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 
2013/2014, ambapo pia siku hiyo ya sherehe za tuzo itatangazwa zawadi ya
 Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa 
katika masuala mbalimbali ya kimichezo hapa nchini. Tuzo hizo ni kuanzia
 Juni 2013 hadi Juni 2014.
ORODHA KAMILI YA WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2013/2014
OLIMPIKI MAALUM:
Wanaume: Raphael Kalukula, Pazi Mwinyimkuu na Hatibu Matali
wanawake: Blandina Blasi, Shida Jaha na Mwanaharusi Risasi.
MPIRA WA KIKAPU;
Wanaume:Lusajo Samwel (Oilers), Erick Mchemba (ABC)
wanawake:Sajda Ahmed Lyamaiga(Don Bosco Lioness), Rehema Silomba (Don Bosco Lioness) na Orlyn Titus (Don Bosco Lioness).
MPIRA WA MAGONGO;
Wanaume:Yohana Wilson, Focus Paul, Deep Vaja
Wanawake: Valentina Quarantta, Kidawa Seremala na Mary Mhina
 MPIRA WA WAVU: 
 Wanawake: Yasinta Remmy (Jeshi Stars), Hellena Richard (Magereza) na Teddy  Abwao (Jeshi Stars).
WanaumE: Kelvin Peter Severino (Magereza), Nassoro Sharifu (Jeshi Stars) na Athuman Rupia (Jeshi Stars).
RIADHA:
Wanawake: Zakia Mrisho, Jaqueline Sakilu na Catherine Lange
Wanaume:Alphonce Felix, Dickson Marwa na Fabian Nelson.
 Continue reading →

No comments:
Post a Comment