Mtayarishaji
 wa tamthilia ya Siri ya Mtungi  Louise Kamin kutoka  Shirika Lisilo la 
Kiserikali la  Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) 
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa 
pili na wa mwisho wa tamthilia hiyo. Kutoka kulia kwa Kamin ni Karabani 
(Muongozaji), Cheche (Muigizaji), Jordan Riber (Muongozaji). Kutoka 
kushoto ni Goldliver Gordian (cheusi) na David Michael (Duma). 
Cheche akizungumza katika mkutano huo
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Msimu wa pili wa tamthilia ya Siri ya Mtungi itazinduliwa rasmi Desemba 7 kupitia televisheni ya Taifa (TBC).
Akizungumza jijini jana, 
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka  Shirika Lisilo la 
Kiserikali la  Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) 
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi
 kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin alisema kuwa kukamilika 
kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins 
University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa 
uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya 
Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI.
Alisema kuwa sehemu hii ndiyo 
inatoa majibu ya msimu wa kwanza na kuwataka mashabiki watamthilia hii 
kuangalia TBC kuanza saa 12.30 jioni kupitia TBC.
“Msimu wa kwanza wa tamthilia ya
 Siri ya Mtungi uliwavutia watu wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki na 
kuwaachia maswali kibao na hii imetokana na tamthilia kubeba vionjo 
halisi vya maisha katika jamii na hasa kwa wakazi wa mikoa ya Pwani ya 
Tanzania,” alisema Kamin.
Alisema kuwa mapokeo mazuri 
kutoka kwa watazamaji kuliwapa nafasi ya kuingia katika vipengele saba 
vya tuzo za M-Net Africa Magic Viewers Choice Awards mwaka 2014 ambavyo 
ni TV Series, Make Up, Wardrobe, Art Direction, Sound Editor, Acting, 
and Indigenous Language Series.
“Msimu wa kwanza ulikuwa hewani 
katika vipindi vya miaka miwili tangu mwezi Desemba mwaka jana kupitia 
vituo vya televisheni vya ITV/EATV na baadaye kurushwa hewani kupitia 
DTV, TV1, MNet Africa Magic, Maisha Magic kabla ya msimu huu kupitia 
televisheni ya TBC,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamin, mpaka sasa 
wanajivunia kupata mapokeo mazuri kwenye mitandao ya kijamii na hasa 
facebook kwa kupata mashabiki 200,000 na kwenye YouTube ambapo tumepata 
watazamaji zaidi ya 500,000 kwani tamthilia hii imepata umaarufu mkubwa 
kwa kutazamwa na mashabiki wengi kuliko vipindi mbali mbali vya 
televisheni hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa Siri ya Mtungi ni 
hadithi ya Kitanzania ambapo wametumia siku 86 kukamilisha kurekodi. 
Alisema mbali ya kuwashirikisha waigizaji maarufu kama yvonne Cherie 
maarufu kwa jina la Monalisa, pia imewashirikisha warembo maarufu kutoka
 Miss Tanzania kama Richa Adhia na Jokate Mwegelo.
“Tumetoa ajira kwa waigizaji 60 ambao walipatikana baada ya mchujo wa watu 2,500,” alisema.

No comments:
Post a Comment