TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 15, 2014

Mamia ya watu wazama DR Congo

Miili ya watu 129 imepatikana katika Ziwa Tanganyika baada ya boti kuzama Ijumaa
Miili ya watu wapatao 129 imepatikana kutoka Ziwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya feri kupinduka na kuzama mapema Ijumaa.
Waziri wa Uchukuzi nchini humo Laurent Sumba Kahozi amesema msako unaendelea kuwatafuta watu waliopotea katika ajali hiyo.

Wafanyakazi wa uokoaji waliwapata abiria wakielea katika maji Jumapili, wakiwa katika mapipa ya petroli na vifaa vingine.
Maboti katika eneo hilo mara nyingi hujazaa abiria na mizigo kupita kiasi na ajali kutokea ni jambo la kawaida
Habari zinasema ajali kama hiyo ni za kawaida katika eneo hilo kutokana na boti kujaa abiria na mzigo kupita kiasi.
Maboya ya kujiokoa mara nyingi hayamo katika maboti hayo na watu wengi hawawezi kuogelea.
Maafisa katika jimbo la Katanga wamesema upepo mkali na kujaza abiria na mizigo kupita kiasi kumesababisha boti MV Mutambala, kupinduka.

Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu waliokumbwa na ajali hiyo ambayo ilitokea mapema Ijumaa asubuhi.
Taarifa za awali zilisema watu 26 wamekufa katika ajali hiyo.
Idadi ya watu walionusurika imetajwa kuwa watu 232, wengi wakiwa ni wanaume, amesema waziri wa uchukuzi katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment