BAADHI ya wanafunzi wa
kike katika Shule ya Msingi Nachitulo Wilayani Newala wamewataka wazazi
kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike kielimu kwani kufanya hivyo ni
kumnyanyasa mtoto wa kike kijinsia.
Wanafunzi hao walitoa kilio hicho hivi
karibuni katika mjadala uliofanyika kwenye shule hiyo uliokuwa ukijadili
vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na uelewa wa vitendo hivyo kwa
watoto ili
kuweza kukabiliana navyo.
kuweza kukabiliana navyo.
Mwanafunzi Sofia Damian wa darasa la tano
‘B’ Shule ya Msingi Nachitulo akizungumza katika mjadala huo aliwaomba
wazazi kuacha tabia ya kufanya ubaguzi wa kumjali zaidi mtoto wa kiume
kielimu na kumsahau yule wa kike kwani kitendo hicho ni ukatili wa
kijinsia.
Alisema baadhi ya wazazi eneo hilo
wamekuwa wakibagua watoto kwa kumjali zaidi wa kiume na kuwaacha wa kike
ni ubaguzi mbaya. “…Kitendo cha kufanya ubaguzi wa elimu katika familia
kwa mtoto wa kike na kiume ni unyanyasaji wa kijinsia…yaani kumpeleka
mtoto wa kiume shuleni na kumuacha wa kike nyumbaji hilo ni
unyanyasaji,” alisema Sofia Damian.
Kwa upande wake Sharifa Bakari toka darasa la sita ‘A’ katika shule hiyo alisema ubaguzi wa mtoto wa kike umekua ukianzia ngazi za familia kwa watoto wa kike kuwa na kazi
nyingi nyumbani zaidi ya mtoto wa kiume kitendo ambacho kinatakiwa
kipigwe vita.
Mwanafunzi wa darasa la sita ‘A’ katika
shule hiyo, Mwanahamisi Said aliwataka baadhi ya wazazi na walezi kuacha
utaratibu wa kumlazimisha mtoto wa kike kuolewa kwa taamaa ya mali
(ndoa za utotoni), kwani kitendo hicho pia ni ukatili wa kijinsia.
“..Hata kitendo cha mtu mzima kumlazimisha mwanafunzi kufanya naye
mapenzi ni ukatili wa kijinsia,” alisema Mwanahamisi.
Akizungumza mwongozaji wa mjadala huo,
Suzan Charles kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama
cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) aliainisha matukio ya ukatili wa
kijinsia yanayowapata watoto na kutoa elimu ya kukabiliana nayo kwao,
ikiwa ni pamoja na wao kutoa taarifa mapema sehemu husika endapo watatokewa na hali kama hizo.
Akizungumza awali kabla ya mjadala huo, Mwalimu wa Malezi wa Shule ya Msingi Nachitulo, Blandina Luwongo alisema shule hiyo imefanikiwa kupiga vita vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa kutumia mradi wa elimisha rika jambo ambalo limeondoa kabisa matukio ya mimba kwa wanafunzi.
“…Katika shule yetu hata matukio ya
wanafunzi kutiwa mimba hayapo kwa sasa baada ya elimu ya uelimishaji
rika kutolewa kwa jamii, wanafunzi na walimu eneo hili. Hata hivyo
anabainisha ili kutokomeza kabisa matukio ya unyanyasaji elimu ya
kukabiliana na vitendo hivi kwa jamii haina budi kutolewa kiufasaha na kuacha kujikita kwenye adhabu kwa wakosaji.” Anasema Bi. Luwongo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment